PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Sunday, December 14, 2014

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


Mwandishi wa Mtandao huu Mkoani Morogoro, Dunstan Shekidele akipiga kura yake leo.
Sokoine-Kibaoni, Morogoro: Wananchi eneo la Sokoine-Kibaoni, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mpaka sasa bado hawajaanza kupiga kura mbali na wengi wao kujitokeza huku wengine wakiwa wamekodi magari kutoka Bwawa la Kihonda umbali wa kilomita 20 kwenda kupiga kura lakini mpaka sasa bado hawajapiga kura.
Amana, Ilala: Baadhi ya wananchi wameamua kususia zoezi la upigaji kura katika Kituo cha Amana, Ilala jijini Dar baada ya mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Amama aitwaye Mathias Ijumba kuondolewa katika uchaguzi dakika za mwisho kwa kile kinachodaiwa kuwa si mkazi wa eneo hilo lakini jambo la ajabu jina like liko katika orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura na mgombea huyo ameruhusiwa kupiga kura yake.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamedai jamaa huyo anakubalika sana na huenda ndiyo chanzo cha jina lake kuondolewa.
Dar es Salaam: Wananchi katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanalalamikia utaratibu wa majina unaotumika katika zoezi la upigaji kura linaloendelea, wengi wadai kupata tabu kuona majina yao huku wengine majina yao yakiwa hayapo kabisa katika vituo.
Shariff Shamba, Ilala: Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana.
Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.

Sunday, December 7, 2014

Walimu waandamana Kasulu, Kigoma



Walimu
zaidi ya 200 katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameandamana na
kumpa wakati mgumu mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Masalu Mayaya,
wakishinikiza kulipwa kwa madai yao mbalimbali yanayofikia zaidi ya
shilingi milioni 172.


 

Viongozi wa chama cha walimu pamoja na walimu hao kutoka shule
mbalimbali za sekondari na msingi wamesema kwa muda mrefu wanaidai
serikali fedha za likizo, uhamisho, mapunjo ya mishahara, matibabu na
hawapandishwi madaraja kwa mujibu wa sheria.


 

Walimu hao pia wamemshutumu Afisa Elimu wa halmashauri hiyo Kalugutu
Zuberi kuwa amekuwa kikwazo kwa maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo na
kwamba licha ya serikali kukataza uhamisho wa watumishi bila malipo
halmashauri hiyo imekuwa ikihamisha walimu bila ya kuwalipa.


 

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Masalu Mayaya akizungumza na
walimu hao, ameahidi ofisi yake kushughulikia matatizo hayo kwa haraka
na kwamba tatizo la kuchelewa kwa malipo linatokana na uhakiki wa
viambatanisho na fedha kutoka serikalini.


 

Katika kikao hicho cha pamoja kati ya mkurugenzi wa Kasulu na walimu,
wamekubaliana kupitia upya madai kwa muda wa wiki moja na kuanza kutoa
barua za kupanda madaraja mwezi ujao.

Wednesday, December 3, 2014

ESCROW: BILIONEA NA MMILIKI WA MITAMBO WA KUFUA UMEME AMESEMA HATAKUBALI HATA KIDOGO KUTAIFISHWA MITAMBO YAKE...



Bilionea na mmiliki wa mitambo wa kufua umeme wa 

Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), 

Harbinder Singh Sethi,

amesema hatakubali hata kidogo kutaifishwa mitambo yake 

ya kuzalisha umeme ya IPTL kama ilivyopendekezwa na 

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mjini 

Dodoma 

hivi karibuni. 


Nini maoni yako juu ya hii kauli yake ?

Tuesday, December 2, 2014

Chadema Arusha Yapata Pigo





CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya mapingamizi yake 155 kwa wagombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Jiji la Arusha kutupwa.
 
Mapingamizi hayo yaliwasilishwa kwa Katibu Tawala wilaya ya Arusha na msimamizi mkuu wa uchaguzi, Juma Iddy ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwa ajili ya kusikiliza rufaa.

 
Akitoa uamuzi huo juzi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Daniel Machunda alisema mapingamizi yaliyowasilishwa na Chadema, yalidai kuwa wagombea wa CCM walikuwa hawajadhaminiwa na chama chao.
 
Machunda alisema mbali na hilo, mwisho wa kurudisha fomu ilikuwa Novemba 23 mwaka huu na mapingamizi yote yalitakiwa kuwasilishwa ndani ya siku mbili kuanzia Novemba 24, lakini Chadema waliyawasilisha Novemba 26, hivyo kuwa nje ya muda uliopo kikanuni.
 
“Kwa mujibu wa kanuni ya uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa katika mamlaka za mji za mwaka 2014 (15) (2) kinasema; 

 

“Pingamizi chini ya kanuni ndogo (1) ya kanuni hii itawasilishwa kwa maandishi kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi ndani ya siku mbili tangu kufanyika kwa uteuzi na msimamizi atatoa uamuzi kwa muda usizidi siku mbili kwa kuanzia siku aliyopokea pingamizi hilo’’ alisema.
 
Alisema kwa mujibu wa kanuni hiyo mapingamizi yote ya Chadema yaliyowasilishwa Novemba 26 mwaka huu yalipelekwa nje ya muda na kwa mantiki hiyo pingamizi hizo yametupiliwa mbali.
 
Akizungumzia hali hiyo, Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Feruz Juma alisema

Wednesday, November 26, 2014

Tweets 3 za Dk.Wilbroad Slaa kuhusiana na kashfa ya Escrow



Tulisema hili la Escrow mapema.
Akaunti nyingi zilizopokea hela zilikuwa ni mpya, nyingine hazikuwa hata
na vitabu vya hundi. Hatuliachi….”
  
-“… Ni jambo la kusikitisha sana
kuona hata benki zinazomilikiwa na madhehebu ya dini sasa zimekuwa
sehemu ya kusambaza fedha zilizoibwa…’.
 
-‘…Fisadi anapoachia ngazi bila
kufikishwa mbele ya sheria ni sawa na kupewa mapumziko kwenda kutumia
alichofisadi. Kuachia ngazi tu haitoshi…’.
 
— Dr Wilbrod Slaa (@wilbrodslaa) November 23, 2014

Tuesday, August 5, 2014

Mjumbe wa UKAWA atinga bungeni

Wakati wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wa kususia vikao vinavyotarajiwa kuanza leo mjini Dodoma, mmoja wa wajumbe wake jana aliripoti bungeni na kujiandikisha. 
Mjumbe huyo, Clara Mwatuka ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), alionekana katika Viwanja vya Bunge saa 6:30 mchana akiwa ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo Livingstone Lusinde (Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi).
CUF ni moja ya vyama vinavyounda Ukawa, pamoja na Chadema na NCCR Mageuzi na tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wametangaza kwamba wajumbe wote wanaotokana na umoja wao hawatashiriki vikao vya Bunge hilo.
 
Mwatuka baada ya kujaza fomu maalumu za kujiandikisha, alielekea lango la Magharibi na kuingia kwenye gari la Bwanausi.
Awali, alipoulizwa kwenye Viwanja vya Bunge kuhusu kuwapo kwake Dodoma, alikataa kuzungumza lakini alikiri kujiandikisha bungeni.
 
Baadaye alipoulizwa imekuwaje akajiandikisha ilhali uongozi wa chama chake umesema hawatashiriki, Mwatuka alijibu: “Kwa hapo ni mapema sana kuzungumzia suala hilo, nitazungumza kesho (leo) kule bungeni ukinitafuta.”
 
Hata hivyo, baada ya dakika kama 30 kupita, Mwatuka alimpigia simu mwandishi na kumwambia: “Sasa kuhusu mimi kuja Dodoma, ni kweli kwamba niko hapa maana nasomesha na nilipofika nimeamua kwenda pale bungeni kuripoti.”
 
Aliogeza: “Ila mimi pamoja na kujiandikisha, sitashiriki vikao vya Bunge mpaka hapo tutakapokuwa tumepewa mwongozo, maana tuliambiwa kwamba majadiliano yanaendelea kwa hiyo tukiruhusiwa nitakwenda, vinginevyo sitashiriki kabisa, ndiyo hivyo.”
 
Bwanausi kwa upande wake alisema alimpa lifti Mwatuka kutoka Dar es Salaam baada ya mbunge huyo wa CUF kuomba msaada wa usafiri kwenda Dodoma.
 
“Ni jambo la kawaida, tulionana Dar es Salaam na akaniuliza iwapo ninakwenda Dodoma na mimi kweli nafasi ilikuwapo kwenye gari, kwa hiyo tumekuja naye hadi hapa, sasa zaidi ya hapo mimi sifahamu,” alisema.
 
Wajumbe kutoka Zanzibar na wale wa kundi la 201 ndiyo waliokuwa wengi katika usajili wa jana na wajumbe ambao wanatokana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa kutoka Tanzania Bara wakionekana wachache.
 
Milango yote ya kuingia katika eneo la Bunge ilikuwa imefungwa na kuacha lango moja tu la Magharibi, hali iliyosababisha baadhi ya wajumbe kuhangaika hadi pale walipopata msaada wa polisi waliokuwa wakilinda
Mkutano wa Bunge Maalumu ambao unafanyika kwa mara ya pili, unatarajia kuchukua miezi miwili ambayo wajumbe wake wanapaswa kuitumia kukamilisha kazi ya kupitia sura 15 za Rasimu ya Katiba zilizosalia na kupiga kura kuamua kuhusu sura mbili zinazohusu Muungano.
 
Katika mkutano uliomalizika Aprili mwaka huu, wabunge walikuwa wametumia zaidi ya siku 70 na walifanikiwa kupitia sura ya kwanza na sita ambazo hata hivyo, hazikupigiwa kura.
 
Hadi jana jioni Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta alikuwa akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi, lakini hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu ratiba wala ajenda za mkutano unaotarajiwa kuanza leo.
 
Wabunge wapata ajali
Katika tukio jingine, Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage na Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria wakati wakitokea Tabora kwenda Dodoma kupata ajali.
 
Wabunge hao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri.
 
Akizungumza akiwa katika Wodi Namba 18, Rage alisema amepata majeraha katika bega la kushoto na eneo la nyuma ya mgongo baada ya dereva wa gari walilokuwa wakisafiria kujaribu kulipita lori lililokuwa mbele yao, lakini ghafla lori hilo likaingia katikati ya barabara.
 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya aliwataja majeruhi wengine wa ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Chigongwe, Dodoma kuwa ni Issa Chimwaga (31), Mwanahamisi Ramadhani (34) na dereva John Hoya (32) ambaye hakuuumia.
 
Alisema vipimo vimeonyesha kuwa mbali na kupata majeraha usoni na kichwani, Munde pia amevunjika mkono wakati Rage ameteguka bega la kushoto