PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Sunday, December 7, 2014

Walimu waandamana Kasulu, Kigoma



Walimu
zaidi ya 200 katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameandamana na
kumpa wakati mgumu mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Masalu Mayaya,
wakishinikiza kulipwa kwa madai yao mbalimbali yanayofikia zaidi ya
shilingi milioni 172.


 

Viongozi wa chama cha walimu pamoja na walimu hao kutoka shule
mbalimbali za sekondari na msingi wamesema kwa muda mrefu wanaidai
serikali fedha za likizo, uhamisho, mapunjo ya mishahara, matibabu na
hawapandishwi madaraja kwa mujibu wa sheria.


 

Walimu hao pia wamemshutumu Afisa Elimu wa halmashauri hiyo Kalugutu
Zuberi kuwa amekuwa kikwazo kwa maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo na
kwamba licha ya serikali kukataza uhamisho wa watumishi bila malipo
halmashauri hiyo imekuwa ikihamisha walimu bila ya kuwalipa.


 

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Masalu Mayaya akizungumza na
walimu hao, ameahidi ofisi yake kushughulikia matatizo hayo kwa haraka
na kwamba tatizo la kuchelewa kwa malipo linatokana na uhakiki wa
viambatanisho na fedha kutoka serikalini.


 

Katika kikao hicho cha pamoja kati ya mkurugenzi wa Kasulu na walimu,
wamekubaliana kupitia upya madai kwa muda wa wiki moja na kuanza kutoa
barua za kupanda madaraja mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment