Yes, good news nyingine Tanzania.
Katika ile ahadi ya jitihada za Serikali
kupitia Wizara ya Uchukuzi kuboresha miundombinu za usafirishaji
nchini, leo kuna taarifa nyingine nzuri juu ya kile ambacho Wizara hiyo
imekifanya kwenye sekta ya usafirishaji ambapo yamewasili mabehewa 50
mengine tayari kwa kuanza kutoa huduma.
“… Ile
ndoto tuliyokuwa tunaitegemea kwa muda mrefu sasa imeanza kutimia tuna
vichwa vya treni 13 ambavyoo tunavitegemea muda wowote ambavyo
vitaongezwa nguvu na vile ambavyo vitaongeza nguvu na vile vichwa
ambavyo tunavitengeneza Morogoro, tulianza na vinane tumemaliza
tunaingiza vingine vinane kwa hiyo nguvu ya TRL mnaiona inaanza kuja
polepole…” Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kiparo Kisamfu amesema; “Haya
mabehewa ni kwa ajili ya safari za kwenda Mikoani hususan Kigoma na
Mwanza lakini nia yetu ni kuanzisha treni maalum ambayo unaweza kuiita
deluxe train ambayo tunatarajia itasimama kwenye vituo vikubwa tu,
haitokuwa kama zile treni mbili zinazotembea sasa hivi… Na kwenye
mabehewa haya kila mtu atakaa kwenye kiti chake hakuna mtu atakayesimama
na yatachukua muda mfupi Zaidi kufika Kigoma na Mwanza kama ilivyo sasa
hivi…”
No comments:
Post a Comment