PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI
Showing posts with label HOME. Show all posts
Showing posts with label HOME. Show all posts

Monday, December 15, 2014

Majambazi wavunja Kanisa Katoliki Kilema, wapora



Kundi la watu wanaodhaniwa ni majambazi, wamevamia na kupora fedha taslimu na vitu mbalimbali katika Kanisa Katoliki la Kilema, Jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
 
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 14, mwaka huu, ambapo watu hao wakiwa na vifaa maalumu vya kuvunja milango, walivunja lango kuu la kanisa hilo, kuvunja sanduku la sadaka na kupora vifaa vya kufanyia ibada.
 
Kanisa hilo ni la kwanza kujengwa na Wamisionari wa kwanza Kanda ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Dodoma.
 
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Padri wa Parokia ya Kilema, Damien Temere Mosha, alisema vitu vilivyoibwa ni pamoja na vifaa vitakatifu vinavyotumika katika sikukuu ya Ekaristi.
 
Akizungumza na mwandishi, Paroko wa Parokia ya Kilema, Padri Mosha alisema majambazi hao walivunja kasha la kuhifadhi sadaka na kupora fedha zilizokuwamo, ambazo hazijajulikana thamani yake.
 
Alisema majambazi hao waliiba vifaa vya kunywea divai na komunio, ambavyo ni vya dhahabu. Padri Mosha alisema majambazi hao walivunja kasha maalumu la kuhifadhi vifaa vya ibada na kuiba vile vya dhahabu tu vyenye thamani ya mamilioni ya fedha huku wakiacha vya shaba.
 
Alisema baadhi ya vifaa hivyo vilinunuliwa na wamisionari wa kwanza na vilikuwa na thamani kubwa kwa Kanisa hilo, kwa kuwa viliwakilisha imani katika parokia hiyo na Kanda nzima ya Kaskazini.
 
Kiongozi huyo wa kanisa alibainisha kuwa jambo lililomsikitisha ni namna eneo takatifu la kanisa hilo lilivyoharibiwa vibaya, kwani eneo hilo mara nyingi limekuwa likitumika kwa ajili ya kutolea sakramenti takatifu kwa mujibu wa utamaduni wa Kanisa hilo Katoliki.
 
Aliwataka wakazi wa Kilema na wanaozunguka eneo hilo kuwa na utulivu wakati huu vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi hadi pale waliohusika na tukio hilo watakapokamatwa na kuchukuliwa hatua.
 
Waumini wa kanisa hilo ambao walikusanyika kwa ajili ya sala yao ya kawaida ya Jumapili majira ya saa moja asubuhi, walijikuta wakichelewa kuanza misa wakati uongozi wa kanisa hilo, ukijaribu kutengeneza na kusafisha maeneo yote yaliyoharibiwa na majambazi hao.
 
Nje ya mlango wa kuingilia kutoa sadaka, kulikuwa na damu na inasadikiwa kuwa huenda ni za mmoja wa watu hao waliovamia kanisa hilo alijeruhiwa wakati akijaribu kuvunja mlango huo, ambao hufungwa kwa vitasa imara.
 
Mosha alisema katika tukio hilo, hakuna mtu aliyejeruhiwa au kupoteza maisha. Paroko huyo alitangaza kuwa kanisa litatoa zawadi ya Sh milioni mbili kwa mwananchi yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi hao.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.

Sunday, December 7, 2014

Zari Sextape: My Ex Lover Leaked It

Zari has today morning  blamed her ex lover for leaking the sextape.


zaris
“Life goes exs gotta stay exs and stop doing things for renege,” Zari tweeted shortly after The Red Pepper published pictures of her sextape.
For exclusive pictures and a clear description of how Zari moans in bed, Please hurry and Grab Red Pepper copies of Friday and Saturday from the nearest vendor.
READ MORE ON: ugandaonline.net

Taarifa nzuri leo kwenye usafiri kwenda Kigoma,Mwanza...


Hitachi-Standard-Class-AYes, good news nyingine Tanzania.
Katika ile ahadi ya jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi kuboresha miundombinu za usafirishaji nchini, leo kuna taarifa nyingine nzuri juu ya kile ambacho Wizara hiyo imekifanya kwenye sekta ya usafirishaji ambapo yamewasili mabehewa 50 mengine tayari kwa kuanza kutoa huduma.
“… Ile ndoto tuliyokuwa tunaitegemea kwa muda mrefu sasa imeanza kutimia tuna vichwa vya treni 13 ambavyoo tunavitegemea muda wowote ambavyo vitaongezwa nguvu na vile ambavyo vitaongeza nguvu na vile vichwa ambavyo tunavitengeneza Morogoro, tulianza na vinane tumemaliza tunaingiza vingine vinane kwa hiyo nguvu ya TRL mnaiona inaanza kuja polepole…” Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kiparo Kisamfu amesema; “Haya mabehewa ni kwa ajili ya safari za kwenda Mikoani hususan Kigoma na Mwanza lakini nia yetu ni kuanzisha treni maalum ambayo unaweza kuiita deluxe train ambayo tunatarajia itasimama kwenye vituo vikubwa tu, haitokuwa kama zile treni mbili zinazotembea sasa hivi… Na kwenye mabehewa haya kila mtu atakaa kwenye kiti chake hakuna mtu atakayesimama na yatachukua muda mfupi Zaidi kufika Kigoma na Mwanza kama ilivyo sasa hivi…”

Wednesday, December 3, 2014

ERROR OF ELECTRICITY IN ELEVATOR APPARENTLY NBC CONFUSION DAR


 This error happened summer at 3:30, confusion resulted in staff kuzikimbia Post Office to Old Garden (small picture) .Wateja who suffered the same raid were directed by the leadership to gain access to other branches of the bank. 

The staff are also in the garden Post a Formerly available in front of their building, having fled the confusion that 


some employees of the Bank of NBC, they crossed the road returning to the office after kuzikimbia due to errors electronics happened in the elevator of an emergency at the Headquarters of the bank, the intersection of streets of Sokoine Drive and Azikiwe, Dar es Salaam today. 

 Employees of the Bank were returned to office after security assurances summer at 4: 35 am 

Staff first aid with their equipment ready to provide the service. However, according to the Jump busy said no employee nor a customer who was injured during the confusion that. 

Head of the Division of Marketing and Communications of the bank, Jump busy (center) was wasilinana different people after the security situation will turn
Head of Marketing and Communications NBC, Jump busy (second right) zungmza and the authors of the information on this confusion.

Tuesday, December 2, 2014

Hatimaye Diamond Aongelea Kuhusu Kuachana na Wema na Mahusiano yake na Zari Boss Lady



diamond na zari
Jana Nov 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:
Adam Mchomvu :”…Nataka kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?“
Diamond :- “… Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…“
B 12  :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?…”
Diamond  :- “…Kuna vitu vitu fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri… Lakini ikifikia kuvizungumzia vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni kwamba kila mtu anafahamu… Haijafikia kuweka wazi ndio maana ninapoulizwa inakuwa ni swali gumu kulijibu.. “
B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…“
Diamond  :- “… Sijui…“
B 12  :- “…Hii ngoma kama umemzungumzia yeye direct hivi… watu wamekuza akili zao zikaenda mbali zaidi kimawazo lakini, kwamba inawezekana ile singo umemwimbia yeye hivi kwamba bado unamzimia japokuwa bado kama kakutosa hivi…“
Diamond  : “.. Waswahili wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu ukisikiliza ile nyimbo kama kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa hauwezi kuwa na maswali mengi …“
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:
Diamond  :- “.. Zari ni rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka kuleta roho za kibaguzi, unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na mimi karibu ili hata kesho na kesho kutwa  mimi nikiwa Nigeria basi Davido anipokee hivyo hivyo…“
Iko hapa full Interview ya Diamond kwenye XXL, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.

Mvua Iliyonyesha Jijini Mwanza Yasababisha Mafuriko


Mvua kubwa iliyonyesha asubuhi ya leo jijini Mwanza, imesababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo kama inavyoonekana pichani.
Baadhi ya
wakazi wa jiji hilo hawana sehemu za kukaa baada ya maji kuingia kwenye
nyumba zao na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.


 
 

Al Sabab Yaua Watu 36 Nchini Kenya





Takribani watu 36 wanahofiwa kufariki katika shambulio lililotokea
kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limethibitisha.


Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu
wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo
yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.


Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu
wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.

Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab limekiri kuhusika na mauaji hayo.

Wednesday, November 26, 2014

Ripoti Ya Escrow.....Leo ndio Leo!!



Ripoti itakayowasilishwa bungeni hii hapa.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiilinda ripoti hiyo usiku kucha.
Wajumbe wa kamati wakiipitia ripoti hiyo kabla ya kuwasilishwa leo bungeni.

**
LEO ndiyo siku iliyokuwa ikisubiriwa baada ya mbinu za kila aina za
kutaka kuzuia mjadala wa ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya IPTL ambapo
Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) itawasilisha bungeni maoni yake
kuhusu ripoti ya kuchotwa zaidi ya shilingi bilioni 321 katika akaunti
ya Tegeta Escrow.

Monday, August 4, 2014

"Siwezi kujadili upuuzi huu" asema Rais Kikwete kuhusu tetesi kuwa alimuokoa Ridhiwani baada ya kukamatwa na dawa za kulevya!





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Sina muda kujadili upuuzi huu kuhusu Ridhiwani – Rais Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni mkusanyiko wa upuuzi mtupu madai kuwa yeye Rais alishiriki kumwokoa mtoto wake, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ambaye alikuwa amekamatwa na madawa ya kulevya nje ya nchi.
 
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Urais ni taasisi kubwa sana nchini na hivyo yeye akiwa Rais hawezi kujiingiza katika ubishani na watu wa mtaani, kama ambavyo wanataka baadhi ya watu wanamsukuma ili ashiriki katika maneno hayo ya mitaani.
 
“This is nonsense – ni mkusanyiko wa upuuzi. Sina muda wala siwezi kupoteza nguvu yangu kujadili upuuzi na ujinga wa namna hiyo,” amesema Rais Kikwete usiku wa Jumamosi, Agosti 2, 2014, wakati alipozungumza na Watanzania wanaoishi katika Marekani kwenye Hoteli ya Marriot Washington, mjini Washington D.C.
 
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa  Marekani alitoa majibu hayo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu madai yaliyotolewa Julai Mosi, mwaka juzi, 2012 na Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA, Wilbroad Slaa, madai hayo yamempeleka mahakamani.
 
Amesema Rais Kikwete: “Hatuwezi sisi kujiingiza katika shughuli ya kupoteza muda kwa kushiriki upuuzi na ujinga. Haya ni maneno ya kipuuzi yanayosemwa na watu ambao kazi yao usiku na mchana ni kuota jinsi ya kuyumbisha ajenda yetu ambayo imefanikiwa sana katika kubadilisha hali ya maisha ya Watanzania.’
 
Amesisitiza Rais Kikwete: “Urais ni taasisi kubwa sana. Rais wa nchi yetu hawezi kujiingiza katika ubishani na watu wa mitaani. Kwanza huyo Ridhiwani amemfikisha Slaa kortini na mpaka leo hata kesi yenyewe haijatajwa.”
 
Kuhusu swali jingine aliloulizwa kuhusu suala hilo, kuwa Rais Kikwete alitia saini mikataba 12 na uongozi wa Jamhuri ya Watu wa China kama sehemu ya masharti ya kuachiwa kwa Ridhiwani, Rais Kikwete amesema:
 
“Naipenda nchi yangu kiasi cha kwamba siwezi kufikiria hata kuiweka rehani. Haya ni maneno ya kipuuzi tu, yenye kutafuta kututoa kwenye ajenda zetu nzuri. Hatuna muda nayo, sisi tunaelekeza nguvu zetu kwenye mambo ya maana ya kuleta mabadikio katika ustawi wa Watanzania.”


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam

ANGALIA PICHA ZA MBUNGE RAGE APATA AJALI AKIWA NJIANI KUELEKEA DODOMA

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) Ismail Aden Rage, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Rufaa, Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014. Rage alipata ajali eneo la Chigongwe, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, wakati akielekea mjini humo tayari kushiriki vikao vya Bunge Maalum vinavyoanza Jumanne Agosti 5, 2014 

Mbunge wa Sikonge mkoani Tabora kupitia CCM, ambaye pia ni Mujumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Nkumba, akimjulia hali Rage, hospitalini mjini Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014.