Mwandishi wa Mtandao huu Mkoani Morogoro, Dunstan Shekidele akipiga kura yake leo.
Sokoine-Kibaoni, Morogoro:
Wananchi eneo la Sokoine-Kibaoni, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mpaka
sasa bado hawajaanza kupiga kura mbali na wengi wao kujitokeza huku
wengine wakiwa wamekodi magari kutoka Bwawa la Kihonda umbali wa
kilomita 20 kwenda kupiga kura lakini mpaka sasa bado hawajapiga kura.Amana, Ilala: Baadhi ya wananchi wameamua kususia zoezi la upigaji kura katika Kituo cha Amana, Ilala jijini Dar baada ya mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Amama aitwaye Mathias Ijumba kuondolewa katika uchaguzi dakika za mwisho kwa kile kinachodaiwa kuwa si mkazi wa eneo hilo lakini jambo la ajabu jina like liko katika orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura na mgombea huyo ameruhusiwa kupiga kura yake.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamedai jamaa huyo anakubalika sana na huenda ndiyo chanzo cha jina lake kuondolewa.
Dar es Salaam: Wananchi katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanalalamikia utaratibu wa majina unaotumika katika zoezi la upigaji kura linaloendelea, wengi wadai kupata tabu kuona majina yao huku wengine majina yao yakiwa hayapo kabisa katika vituo.
Shariff Shamba, Ilala: Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana.
Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.
No comments:
Post a Comment