London, England. Kocha Jose Mourinho amesema kamwe hawezi
kufanya mambo yake katika usajili kwa kuwaiga mahasimu wao, Manchester
United, ambao wanatumia fedha nyingi kwa sasa.
Chelsea ilianza usajili wao mkubwa kwa kuwanasa nyota wa Hispania, Diego Costa na Cesc Fabregas mapema kabla ya Kombe la Dunia.
Lakini bosi huyo wa Chelsea alisema hata katika
usajili wa Januari atarudia alichofanya awali kwa kuwa miamba hiyo haiko
tayari kwa sasa kutoa fedha zaidi katika usajili.
Mourinho alihusisha sheria ya uungwana katika
matumizi kuwa inaweza kuifunga Chelsea kwa kuwa timu inayoweza kutumia
fedha zaidi, huku akisisitiza kuwa hawawezi kufikia rekodi ya Pauni 60
milioni iliyowekwa na United walipomsajili Angel Di Maria. Usajili wa Di
Maria ulivunja rekodi iliyowekwa na Chelsea 2011 ilipomsajili Fernando
Torres kwa Pauni 50 milioni.
“Tunatengeneza fedha ili tuweze kuzitumia. Katika
kila dirisha la usajili Chelsea inapoteza wachezaji, inauza wachezaji,”
Mourinho aliliambia Eurosport.
Matumizi ya Chelsea yako mbali na ya Manchester
United, ambao wametumia fedha nyingi kusajili wachezaji kama Di Maria na
Luke Shaw msimu huu, wakati Blues wakitumia Pauni 30 milioni za mkataba
wa kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas, ambapo inazidiwa na Pauni 75
milioni wanazopata United katika udhamini.
Lakini Mourinho hana tatizo katika mpango wake wa
kusitisha matumizi ya fedha kutokana na kulizoea hilo alipokuwa na klabu
ya Porto.
“Chelsea kwa sasa si watumiaji wa fedha nyingi.
Kwa sasa tunatengeneza fedha nyingi katika dirisha la usajili kuliko
tunazotumia kununua wachezaji.
“Hivyo kwa sasa Real Madrid, Barcelona, Bayern,
Manchester (United) ndizo zinazotumia fedha nyingi, nadhani wana nafasi
katika hilo,” alisema.
No comments:
Post a Comment