PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Monday, September 8, 2014

Sarafu ya Sh500 kuanza kutumika Oktoba


Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezindua rasmi sarafu mpya ya Sh500 itakayoanza kutumika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kutambulisha sarafu hiyo, mkurugenzi wa huduma za kibenki wa BoT, Emmanuel Boaz alisema Serikali imefanya uamuzi huo ili kurahisisha upatikanaji wa chenji na kutunza ubora wa fedha.
“Noti ya Sh500 ndiyo inayopitia mikononi mwa wananchi wengi hivyo kuchakaa mapema. Lakini kutokana na gharama ya kuzichapisha ukilinganisha na sarafu ambazo hudumu kwa muda mrefu, tumeamua kuziondoa noti na kuleta sarafu yenye thamani ile ile.
Kuna taratibu tunaendelea kuzikamilisha kabla hatujaziingiza sarafu hizo katika mzunguko mwezi Oktoba. Zitakapoanza kutumika hakutakuwa na haja ya wananchi kwenda kubadilisha noti walizonazo kwani zitakuwa zinatumika pamoja hadi zitakapopotea katika mzunguko,”alisema.
Sarafu hiyo ina umbo la duara, lenye kipenyo cha milimita 27.5 na michirizi pembeni ikiwa na uzito wa gramu 9.5. Mbele ina picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume na nyuma ni nyati.

 

No comments:

Post a Comment