PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Thursday, October 10, 2013

MWANAMKE ACHOMA TUNGULI NA UGANGA WA MUMEWE.

Mwanamke achoma tunguli na uganga wa mumewe.
Tukio hilo limetokea jana siku ya jumatano, majira ya saa saba mchana katika Mkoa wa Dar es salaam, wilaya ya Ilala, kata ya chanika, eneo liitwalo kwa Ngwale, ambapo nilipata fursa ya kushuhudia tukio hilo na kuwahoji wahusika. Mwanamke huyo aliyeamua kuchoma tunguli zote, manyanga, singa, hirizi na dawa mbalimbali pamoja na kibanda cha uganga cha mumewe ambaye ni mganga wakienyeji, alikuwa na haya ya kusema"Nimemvumilia sana nimechoka, amezidi kuninyanyasa sana huyu mwanaume, kilasiku ananipiga, hanipi haki yangu kama mkewe, kila siku anafanya utapeli tu akijifanya mganga, hana uganga wowote ule, nimechoka na manyanyaso yake, najua kinachompa jeuri ni huu uganga wake feki, sasa nimechoma moto kilakitu, nione jeuri yake itakuwa wapi" alisema mwanamke huyo akiwa na jazba kali.

Nilipojaribu kumhoji mganga huyo wakienyeji, yeye hakuwa tayari kutoa ufafanuzi wowote kwa muda ule, bali alisema tu kuwa "naomba uniache kwa sasa, nimechanganyikiwa sijui nitafanyaje, sikutegemea huyu shetani (mke wake) angefanya huu upuuzi. Atajuta maisha yake yote, ametafuta ugomvi ambao hataweza kuumaliza".
Tukio hilo lilishuhudiwa na watu wengi waliotaka kujua nini kingetokea baada ya kibanda cha uganga kuchomwa moto, na wala si kutoa msaada wa kuzima moto huo. Nilipenda kujua zaidi kuwa je, wanandoa hao wangeweza kukaa na kumaliza tofauti zao hata baada ya tukio hilo, lakini mganga yule wa kienyeji alisema. "Mc Mgonja nakuomba usitake kujua zaidi kwani huyu mwanamke kwa hili tukio la leo, ameweka maisha yangu na yake hatarini, sijui kama tutakuwa salama, huu sio muda wa kutafuta suluhu, bali ni muda wakutafuta uhai kwanza kwani waweza kututoka muda wowote"

Nilipomuuliza mwanamke juu ya hofu ya kifo kwa kosa la kuchoma uganga wa mumewe, yeye alikuwa na haya ya kusema " mimi siamini uchawi wala uganga, siogopi chochote kile, mumue wangu kwani mganga kweli? Hana lolote tapeli mkubwa tu, kama kweli uganga wake unafanya kazi utanidhuru" baada ya kusema hayo mwanamke yule alipanda bodaboda na kuelekea kwa dadayake anayeishi mkoa wa Pwani, wilaya ya Kisarawe.
Nilijaribu kumhoji zaidi mganga yule iwapo angetafuta uganga mwingine na kuendelea na kazi yake ya uganga, lakini swali hilo halikujibiwa badala yake alikuwa mkali, akanigeuzia kibao na kutaka kupasua Ipad yangu ili kupoteza ushahidi wa picha. Hivyo nilijitetea kwa kufuta picha zote za tukio, lakini hakufanikiwa kufuta kumbukumbu yangu iliyopo kichwani.

Hili ni tukio la kweli kabisa na nikizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa majirani wa mganga huyo leo asubuhi, ameniambia kuwa mpaka sasa Mganga huyo hajulikani alipoenda, na hatua za kumtafuta zinafanywa na majirani wanaotaka kujua tu nini kitatokea baada ya tukio lile. Nikikuletea tukio hili lakusisimua, ni mimi Mhabarishaji wako Mc Mgonja.
Kwa habari na mtukio mbalimbali wasiliana nami kwa namba 0713651858.

No comments:

Post a Comment