WAZIRI wa
Ujenzi, Dk John Magufuli amesema miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara
inayoendelea nchini na yenye urefu wa kilometa 11, 154, imetoa ajira kwa watu
650,000.
Aidha, Dk
Magufuli amesema ujenzi huo mkubwa wa barabara, ndiyo tafsiri sahihi ya
kaulimbiu maarufu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Maisha Bora kwa Kila
Mtanzania.
Dk Magufuli
alisema tofauti na mawazo ya baadhi ya watu, miradi hiyo mikubwa ya ujenzi wa
barabara inagharimiwa kwa asilimia 60 na Serikali ya Tanzania.
Waziri
Magufuli aliuambia mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika kijiji cha Nanja
mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa mradi wa ukarabati mkubwa wa Barabara ya
Minjigu-Arusha kuwa miradi ya ujenzi pekee yake imezaa ajira 650,000. Wananchi
pengine watu hawajui, lakini nataka kuwaelezeni kuwa katika Wizara moja tu ya
Ujenzi kiasi cha ajira 650, 000 zimepatikana kutokana na miradi mikubwa ya
barabara inayoendelea kujengwa nchini ya kiasi cha kilomita 11,154,” alisema Dk
Magufuli Kuhusu maisha bora, alisema “Watu wanakejeli kaulimbiu ya maisha bora,
lakini sisi katika CCM tunaposema maisha bora hakuna maana ya Serikali kugawa
fedha kwa wananchi, bali ni Serikali kuwezesha wananchi. Maisha bora ni
barabara, maisha bora ni usafiri wa wananchi wa uhakika kwenye barabara za
lami, maisha bora ni usafirishaji mizigo usiokuwa na matatizo. Haya ndiyo
maisha bora”
Aliwaambia
wananchi kuwa uwezo wa Serikali kuhudumia barabara na kujenga barabara hasa za
vijijini umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka saba iliyopita
Wakati
uongozi wa sasa unaingia madarakani mwaka 2005, Mfuko wa Barabara ulikuwa na
kiasi cha shilingi bilioni 54, lakini mwaka huu, kiasi hicho kwenye Mfuko huo
kimefikia shilingi bilioni 430. Haya ni mafanikio makubwa sana na yanaongeza
uwezo wa Serikali kuhudumia na kujenga barabara,” alieleza. Wakati huo huo,
Rais Jakaya Kikwete janai alizindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mikoa
ya Arusha na Manyara, ikiwa ni sehemu ya ziara zake za kukagua na kuzindua
miradi ya maendeleo katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida.
No comments:
Post a Comment