POLISI mkoani Mwanza inamshikilia Mganga wa Zahanati
ya Kiloleli katika Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela, Dk Lameck Msafiri kwa
kusababisha kifo cha mtoto wa miaka 15 wakati akimtoa mimba.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lily Matola
alisema Msafiri alisababisha kifo cha mtoto huyo juzi saa 3 usiku
Kwa mujibu wa Kamanda Matola, mimba ya mtoto huyo
ilikuwa ya miezi minne na kabla ya kuaga duniai, alikuwa akiishi na wazazi wake
katika eneo la Kilimahewa, jijini hapa. Matola alisema Dk Msafiri anashikiliwa
kwa mahojiano zaidi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Wakati huo huo, wanafunzi 30 wa Shule ya Msingi Lake B
pamoja na mwalimu wao wamenusurika kufa baada ya kujeruhiwa na radi kali
iliyopiga juzi saa 4 asubuhi wakati wakiwa darasani
Kamanda Matola alisema ajali hiyo ilitokea wakati
wanafunzi hao wa darasa la pili wakiwa darasani pamoja na mwalimu wao
Alisema walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya
Mkoa ya Sekou Toure kwa matibabu. Alisema mwanafunzi Felix Revocatus (8) hali
yake sio nzuri na amelazwa hospitalini hapo huku wengine wakitibiwa na
kuruhusiwa.
Katika tukio jingine, mvua kubwa inayoendelea kunyesha
jijini Mwanza imesababisha kifo cha mtoto wa miezi mitatu, Ashfat Abdsalama
baaada ya mtoto huyo pamoja na wazazi wake kuangukiwa na ukuta wa nyumba
wanayoishi wakati wakiwa ndani Akifafanua Kamanda Matola, alisema juzi saa 4
asubuhi katika eneo la Kirumba Mlimani B, Abdsalama Hussein (30) na mkewe
Nardia Geresheni (25) pamoja na mtoto wao, walidondokewa na ukuta wa nyumba
baada ya ukuta huo kudondokewa na jiwe Alisema majeruhi hao walipelekwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu, lakini baadaye mtoto huyo alifariki
dunia na hali za baba na mama pia sio nzuri.
No comments:
Post a Comment