Radamel Falcao Garcia, alizaliwa 10-02-1986 katika jiji la Santa Marta, nchini Colombia. Jina lake la utani Mfalme wa Europa, kutokana na kiwango cha ajabu alichokionesha katika michuano hiyo. Falcao akiwa katika timu ya U-17 nchini Colombia, aliteka hisia za timu ya River plate ya nchini Argentina ambapo alimsajili wakati alipokuwa akiendelea na masomo yake ya uandishi wa habari katika chuo cha Parlemo. akiwa na umri wa miaka 19, alifunga magoli mawili katika mechi ya kwanaza aliyochezea timu yake ya River Plate mwaka 2005. alipata majeraha na kwa muda mrefu. mwaka 2007 Falcao alirejea na alifunga magoli natatu katika mechi moja. aliendelea kuonesha uwezo wake na hatimaye katika mechi ya wapinzani wa jadi kati ya River Plate na Boca Juniors iliyopigwa 07-10-2007, alifunga goli muhimu katika mchezo huo. tangu hapo Falcao amekuwa tegemeo katika timu ya taifa ya Colombia.
Tarehe 15-07-2009 Falcao alihamia Fc Porto kwa ada ya uhamisho paun milion tatu.aliibuka kuwa mfungaji bora wa pili wa ligi ya ureno kwa kufunga magoli 25. akiwa na timu ya porto aliiwezesha kutwaa taji la ligi ya Europa akiwa amefunga magoli 17. Tarehe 18-08-2011 Falcao alimaliza msimu kwa kufunga magoli 34. katika mashindano yote katika msimu huo. 2010-2011 Falcao alifunga magoli 17 katika michuano ya Europa na kufunika record ya Jurgen Klinsmann ya goli 15 katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment