vijana wawili wenye umri wa miaka 14 na miaka 12 ndio wamesababisha hali kutokuwa shwari Mbagala. Chanzo cha fujo hizo ni mabishano ya madogo wawili wenye imani tofauti mmoja akiwa ametoka madrasa akaenda uwanjani kuangalia watu wachezao mpira, hapo akakutana na kijana mwingine ambapo wakaanza mabishano ya dini, yule mwenye imani ya kiislamu akimwambia mwenzake kwamba eti ukikojolea msaafu unakua chizi yule dogo mwingine kaukojolea kweli na hajawa chizi, Yule mwenzake alivyoona kashindwa ikabidi aende msikitini akawatonya waislamu kwamba kuna dogo kakojolea msaafu, Si unajua tena wakatoka waislamu wenye siasa kali wakataka kumuua dogo polisi wameingilia kati na kumuokoa huyo dogo sasa ni vita ya mabomu ya machozi ya Polisi na mawe yanayorushwa na watu manaodhaniwa kuwa wenye imani ya kiislamu, Hali sio shwari kabisa magari kibao yamevunjwa vioo na fujo bado inaendelea mpaka sasa.
Hali kama hii sio nzuri ikiendelea kwani sisi watanzania hatupaswi kufikia huko. kamanda wa kanda maalumu Kova amezungumzia tukio hilo na akalifafanua vyema akisema "uchunguzi unaendelea kufanyika lakini mpaka sasa imeonekana kuwa hakuna sababu ya kupandikizwa kuhusu tukio hilo, bali ni utoto na akili za watoto waliokuwa wanabishana. watanzania tusilichukulie jambo hili kwa namna isiyo ya kawaida, nawasihi watanzania waelewe kuwa hilo ni jambo lililopo mikononi mwa vyombo vya dola".
Watanzania tuwe wavumilivu kwani migogoro ya dini kama hii imezipelekea nchi nyingi kupoteza amani ambayo hawajaweza kuirudisha tena mpaka sasa. jamii ijaribu kuelewa chanzo ni ubishani wa watoto hao wawili, ni jambo linaloeleweka hivyo hakuna haja ya kufanya vurugu.
No comments:
Post a Comment