PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Sunday, October 7, 2012

MECHI ZA VISASI KUPIGWA LEO


Manchester united itakuwa na kibarua kigumu cha kusaka point kwa Newcastle ambao wamekuwa na kikosi kizuri kanacho ongozwa vyema na mshambuliaji Demba Ba, ambaye amekuwa na uchu wa magoli. hii ni mechi itakayokuwa na mvuto kuitazama pia kwani mshambuliaji wa man u, R. Vanpersie nae yupo vizuri. kocha wa man u, ameuzungumzia mchezo huu akisema " Newcastle ni timu nzuri, na ina washambuliaji wazuri, lakini sisi pia tuna wachezaji bora zaidi, tutajitahidi kupata ushindi". mchezo huu utapigwa majira ya saa kumi na mbili jion.






mechi yenye kuteka hisia za mashabiki wengi wa ufaransa itazikutanisha Marseille na PSG, huku ukitegemewa kuwa mchezo wenye mvuto wa aina yake kwani, timu zote hizo zipo katika kiwango cha hali ya juu. PSG inatazamwa kwa jicho la tatu hasa kutokana na kumilikiwa na mabilionea ambao wameitumia pesa kusajili vile walivyopenda. mchezo huu utapigwa majira yasaa nne kamili.

vita nyingine ni kati ya Ac Milani na Inter milan, ambazo zitambana leo katika uwanja wao wa nyumbani. hii ni mechi ya wapinzani wa jadi na mara nyingi matokeo ya mechi hii huwa haya angalii sana fomu za timu husika. ni mchezo utakaozikutanisha timu hizo huku zikiwa hazipo katika kiwango bora, ikilinganishwa na misiu mingine. mchezo huu utapigwa majira ya saa tatu na nusu.




  Barcelona itakuwa nyumbani leo ikiwakaribisha mahasimu wao wakubwa Real Madrid, katika mchezo unaotazamiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kama ambavyo imezoeleka. barcelona haijapoteza mchezo hata mmoja, imeshinda mechi nane na kujichukulia points 24. Real Madrid hawakuanza msimu huu vizuri lakini nao wamerudi katika kiwango kizuri kwani katika mechi mbili za mwisho imeweza kufunga magoli tisa.  Vita nyingine itakuwa kati ya Lionel Messi na Christiano Ronaldo, ambao wameendelea kuchuana vikali kwani kila mmoja ameshafunga magoli sita katika ligi, wanachuana vikali kuhakikisha kila mmoja anaibuka kuwa mchezaji bora.




  




No comments:

Post a Comment