PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI
Saturday, October 6, 2012
MATOKEO YA MECHI ZA LIGI YA ENGLAND. CHELSEA , WBA ZAUA.
Chelsea imezidi kujikita kileleni, baada ya kuitandika Norwich bao 4-1. Alikuwa ni Grant Holt aliyezifumania nyavu za chelsea kunako dakika ya 11. Fernando Torres ndiye aliyefungua karamu hiyo ya magoli kunako dakika ya 13. Frank Lampad aliachia mashine safi sana kunako dakika ya 22 nakufanya matokeo kuwa mbili bila. dakika ya 31 Eden Hazard aliiandikia chelsea bao la tatu. Branislav Ivanovic alimaliza karamu hiyo kwa kupachika goli zuri kunako dakika ya 75.
Swansea yatoshana nguvu na Reading kwa bao 2-2. ulikuwa ni mchezo uliotawaliwa na kasi hasa baada ya reading kutangulia kupata magoli mawili kunako dakika ya 30, goli llilowekwa kimyani na Pavel Pogrebnyak. dakika ya 44, Noel Hunt aliipatia Reading goli la pili. Swansea walijipanga vizuri na dakika ya 71, Michu aliifungia swansea na kunako dakika ya 78 Wyne Routledge aliisawazishia swansea goli la pili.
West Bromwich Albion imeendelea kufanya vizuri kwa kuitandika QPR 3-2. Ilikuwa ni mechi yenye presha ya hali ya juu hasa kwa kocha Mark Hughes ambaye kibarua chake kimeendelea kuwa na mashaka kutokana na kufanya vibaya katika ligi.James Morrison aliipatia WBA goli la kuongoza kunako dakika ya 4. alikuwa ni Zoltan Gera alyeandikia WBA goli la pili kunako dakika ya 21. QPR waliamka na dakika ya 35 Adel Taarabt aliipatia goli. kunako dakika ya 82 Youssufu Mulumbu aliipatia WBA goli la tatu. dakika ya 92 Esteban Granero aliipatia QPR goli la pili,lakini haikusaidia kitu kwani kipigo kilibaki palepale.
Wigan athletic imetoshana nguvu na Everton 2-2. ilikuwa ni wigan iliyoanza kufumania nyavu dakika ya 10, kupitia kwa Arouna Kone. Everton wakasawazisha kupitia Nikica Jelavic dakika ya 11. Wigan wakaongeza goli dakika ya 23 kupitia kwa Franco Di Santo. Everton walpata penalt na Leighton Baines akaisawazishia kunako dakika ya 86.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment