Aidha mgeni rasmi aliwasihi vijana wa chama cha mapinduzi kutojihusisha na mapenzi kwanza kabla hawajajiimarisha kiuchumi, pia aliwaasa vijana hao kuepuka ngono zembe na kuwa makini na afya zao, aliwahimiza kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa Taifa ikiwa ni pamoja na kujiandikisha katika daftari la kudumu ili wakati ukifika waweze kuchagua viongozi makini wa chama cha mapinduzi. Zungu alichangia fedha kiasi cha sh million mbili katika mfuko wa maendeleo wa chama cha mapinduzi chuo cha CBE, na kuahidi kushirikiana nao katika maswala yote ya kiuchumi kwa kuwasihi watumie elimu waliyonayo kujiajiri na akawaambia kuna fedha za mfuko wa maendeleo wa jimbo ambazo zinahitaji kutumika, hivyo vijana watumie vizuri fursa hiyo.
Comrade Emmanuel Mgonja akizungumza kwenye mahafali hayo
Comrade Mgonja amewasihi Vijana 1.kujitokeza Kwa wingi kwenye zoezi la kujiandikisha ili wakati ukifika wawe na haki ya kupiga kura.
2. Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Maendeleo kwani Taifa linawategemea
3. Kusoma na kuielewa katiba pendekezwa ili ukifika wakati muafaka waweza kuipigia kura ya ndio.
4. Kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wakiwa na nia ya dhati ya kuboresha pale ambapo waliopita waliishia
5. Kutokubali kushiriki katika siasa chafu zenye uchochezi ambazo ni hatari katika Amani ya Taifa letu.
6. Kutokubali kutumiwa na viongozi wa vyama Vya upinzani katika vitendo viovu Kama maandamano yasiyo halali, kushiriki katika mbinu chafu za uhalifu na uvunjaji wa sheria.
7. Kutumia elimu waliyonayo katika kujiajiri na kukuza uchumi badala ya kukaa na kulalamika kuwa hakuna ajira.
Aidha comrade Mgonja alimaliza Kwa kusema kuwa atawania nafasi ya udiwani wa Kata ya Msasani. Na akawasihi wana cbe kumuunga mkono wakati utakapofika.
No comments:
Post a Comment