PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Monday, March 30, 2015

AMKA KIJANA USIBWETEKE

CHUMA USIPOKITUMIA KWA MUDA KINAOTA KUTU
Kwa wale ambao wamesoma chemistry japo kidato cha kwanza watakuwa wanaijua hii sentesi, hivyo ndivyo ilivyo na maisha ndivyo yalivyo.Tatizo sio mshahara mdogo, tatizo sio ajira hakuna, tatizo sio fursa, tatizo sio kusoma mchepuo wa hati au sayansi, tatizo sio wazazi wako, tatizo ni akili yako umeshindwa kuitumia sasa imeota kutu.

Hebu fikiria vijana wangapi wapo mtaani wanasubiri ajira leo mwaka wa tatu tangu wamalize chuo, nafikiri unakumbuka zile nafasi kumi za uhamiaji zilizotangazwa wakaenda watafuta kazi zaidi ya elfu kumi, ni kweli kusoma huenda haujui lakini hata picha huoni, yani hujiulizi nafasi kumi zinagombaniwa na wati 10000, hayo ni madhara ya kutokutumia akili vizuri matokeo yake imeota kutu bado unajipa moyo uendelee kukaa nyumbani ipo siku utapata kazi.

Amka kijana acha kuifanya akili yako kuota kutu mbona vipo vitu vingi vya kufanya tofauti na ajira, mbona zipo fursa nyingi wenzio tumezichangamkia na ajira imebaki story, hebu jiulize mara ya mwisho umesoma lini kitabu cha mtu aliefanikiwa, mara ya mwisho umehudhuria semina ya  mafanikio na ujasiriamali, mara mwisho lini kuangalia video inayozungumzia mafanikio, huenda hata ninachokizungumzia hukijui.acha kuufanya ubongo wako kuwa na kutu halafu ukitegemea uwe na thaman.

Nikuulize na wewe ulieingia kwenye ajira tangu 2000 hadi leo akili yako inawaza NSSF ndio uanzishe biashara, utakumbuka shuka asubuhi imefika, huu ndio wakati wako wa kuanza kujipanga, hujasoma kitabu tangu utoke chuo, siku tofauti tofauti wenzio wanaenda kwenye semina na mikutano ya mafanikio wewe ndo unaseries za muvi, unadhani utafanikiwa kwa kuendelea kupiga kelele mshahara hautoshi? Fyuuuuuu😣😣😣 acha kulala wakati wenzio tumeamka.maisha yamebadilika, na fursa zimefunguka na watu tunazitumia.

Na wewe uliekata tamaa mapema ngoja nikuulize hivi dhahabu isipochomwa moto itang'aa, jibu unalo na maisha ndivyo yalivyo hakuna  vitu rahisi, kila kitu unachokiona kinacholeta mafanikio kinachangamoto, kwanini unakata tamaa, siku zote watu wanaotumia akili zao vizuri hawachoki kutafuta kile wanachokitaka kwenye maisha yao hadi wakipate.Usichoke hata kama utatumia muda mrefu na utakutana na changamoto nyingi.
İ like this, u can also share with yo friends

No comments:

Post a Comment