PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Wednesday, January 14, 2015

MAMBO 30 YA KUKUFANYA UFANIKIWE

Yafuatayo ni mambo 30 unayotakiwa kusema HAPANA kwa mwaka huu 2015.
1. Sema hapana kwa uvivu.
2. Sema hapana kwa tabia ya kuahirisha mambo.
3. Sema hapana kwa tabia ya kufuata mkumbo.
4. Sema hapana kwa tabia ya kulalamika bila sababu.
5. Sema hapana kwa tabia ya kutoa au kupokea rushwa.
6. Sema hapana kwa tabia ya kutokujiwekea akiba.
7. Sema hapana kwa mahusiano ambayo hayakujengi.
8. Sema hapana kwa vipindi vya TV vinavyokupotezea muda.
9. Sema hapana kwa tabia ya kutegemea wengine ndio wabadili maisha yako.
10. Sema hapana kwa tabia ya kukwepa majukumu yako.
11. Sema hapana kwa tabia ya kutafuta njia ya mkato ya kupata mafanikio.
12. Sema hapana kwa tabia ya kutegemea kupata vitu vya bure.
13. Sema hapana kwa tabia ya kusengenya wengine, kupika majungu na umbea.
14. Sema hapana kwa tabia ya kufikiri hakuna fursa.
15. Sema hapana kwa imani kwamba wewe huna bahati.
16. Sema hapana kwa imani kwamba wenye fedha wana roho mbaya.
17. Sema hapana kwa kazi ambayo unaifanya lakini huipendi.
18. Sema hapana kwa biashara ambayo unaifanya lakini inakusumbua.
19. Sema hapana kwa ulevi.
20. Sema hapana kwa tabia ya kufuatilia maisha ya wengine.
21. Sema hapana kwa tabia ya kufanya mambo kwa mazoea.
22. Sema hapana kwa tabia ya kuiga maisha ya wengine.
23. Sema hapana kwa kwa hofu zinazokuzuia kufanya mambo makubwa.
24. Sema hapana kwa tabia ya kutokujiamini.
25. Sema hapana kwa kuendelea kuwa wa kawaida.
26. Sema hapana kwa tabia ya kupoteza muda muda kwenye mitandao.
27. Sema hapana kwa tabia ya kukosa uaminifu.
28. Sema hapana kwa tabia ya kunyanyasa au kukandamiza wengine.
29. Sema hapana kwa tabia ya kufikiri kwamba kuna uhaba wa fedha.
30. Sema hapana kwa tabia ya kuanza mambo na kuishia katikati.
Kuna mambo mengi sana, zaidi ya 100 ya wewe kusema hapana ili uweze kuboresha maisha yako. Anza na mambo hayo 30 na baadae utaendelea kuongeza mengine kadiri utakavyofanikiwa kuachana na hayo. Kumbuka pia huu ni mwaka wa JUST DO IT, yaani kama kuna chochote unataka kufanya ANZA KUFANYA SASA.

No comments:

Post a Comment