PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Monday, December 15, 2014

Rolene Strauss wa Afrika Kusini ashinda taji la Miss World





Miss South Africa, Rolene Strauss ndiye Miss World 2014. Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22 na mwanafunzi wa medical
ameshinda taji hilo kwenye shindano hilo lililofanyika Jumapili jijini
London, Uingereza.
 
Miss Hungary Edina Kulcsar alishika nafasi ya pili na Miss United States, Elizabeth Safrit akishika nafasi ya tatu.
 
Kabla ya ushindi orodha ya warembo walioingia Top 10 ilikuwa ni: Miss
Australia (10), Mexico (9), United States (8), Kenya (7), Hungary (6),
Brazil (5), Guyana (4), England (3), South Africa (2) na India (1).
 
Rolene anakuwa mrembo wa pili kutoka Afrika Kusini kuwahi kushinda taji hilo.
 
Naye mwakilishi wa Tanzania Happiness Watimanywa amempongeza Miss
World na pia kuwashukuru Watanzania kwa jinsi walivyomuunga mkono.
 
“Nampongeza @rolenestrauss (South Africa) kwa kuibuka mshindi Miss World 2014.
 
Watanzania wenzangu na marafiki kutoka mataifa mengine, tumepiga kura
sana, mmeonyesha support kubwa kuliko matarajio ya wengi bahati mbaya
kura hazikutosha.
 
Natumia nafasi hii kuwashukuru wote mmoja mmoja kwa kuniunga mkono kwa
kipindi chote ambacho nilikua hapa jijini #London na tokea niliposhinda
mashindano ya #MissTanzania. Nisingefika hapa bila support yako. From
deep inside my heart. I thank you. 
 
Kuanzia aliyetumia muda na pesa yake kunipigia kura, aliyeandika na
kutangaza habari yangu, designers mbalimbali, familia yangu, marafiki
wote, wote, wote, I thank you. Nimejifunza vitu vingi sana kipindi chote
hiki na kwakweli watanzania tumeonyesha umoja wa hali ya juu sana.
Umoja wetu na udumu katika mambo yote ya kimaendeleo kwa taifa letu.
 
Mbarikiwe
#Happiness4MissWorld.”

1 comment:

  1. titanium arts
    TATONIC nba매니아 ART CUSTOMING www.jtmhub.com · TATONIC ROCKING T-TATONIC 바카라사이트 ROCKING T-TATONIC ROCKING T-TATONIC. This 토토사이트 unique and original design is crafted with the use of sustainable dental implants

    ReplyDelete