PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI
Wednesday, October 23, 2013
FAHAMU SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA
SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA NI ZIPI?
Habari za asubuhi wapendwa wafuatiliaji wa blog
hii! kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa
shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu
kuweza kuniamsha salama nikiwa na afya njema. Mada yangu leo inahusu siku za hatari ambazo
mwanamke akifanya ngono bila kinga basi
anakuwa katika hatari ya kushika mimba. Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua
kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba,
utupaji wa watoto na hata kuwa na watoto wa
mitaani yanasababishwa zaidi na mimba ambazo
hazikutarajiwa ambazo zingine zinatokana na
mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga. Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko
wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika
makundi makuu matatu3 ambayo ni : mzunguko
mfupi(siku25 kurudi nyuma), mzunguko wa
kawaida(siku28) na mzunguko mrefu(siku30-35) Wanawake wengi mzunguko wao huwa ni wa
kawaida yaani siku 28 hawa ndio leo
nitawaongelea zaidi.
NAMNA YA KUTAMBUA MZUNGUKO WAKO.
Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi
unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza kuona
damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu
ya hedhi ya mwezi unaofuata, kwa mfano ukiona
damu ya hedhi tarehe 15 December basi hiyo ndio
siku yako ya kwanza. Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku
zake za hatari za kuweza kushika mimba ni siku ya
kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku
ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza
kushika mimba. Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari
ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12
anaweza akapata mimba?
Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa
kudumu kwa masaa24 hadi 48 baada ya
kujamiiana hivyo kama utafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu
zikiwa hai hivyo zitarutubishwa. kwa leo tuishie hapo mpendwa mfuatiliaji ili
kukuachia nafasi ya kuchangia zaidi na kuboresha
yale ambayo sikuweza kuelezea zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment