Watafiti wa masuala ya uhusiano na ndoa wana kalenda
za miaka ya hatari iliyotafsiriwa sambamba na sababu zinazoweza kuvuruga
uhusiano na kuwafanya watu waliokuwa wakipendana kuachana.
Hivyo kwa dondoo tu nimeona ni vyema niwafundishe watu wanaoishi kwenye ndoa sababu zinazotafsiri ukomo wa mapenzi yao kulingana na miaka husika iliyotafsiliwa na watalaamu wa masuala ya ndoa na uhusiano.
Wanasaikolojia
mbalimbali ulimwenguni kupitia tafiti zao walikubali kuuweka UGOMVI
kuwa katika sababu zinazoweza kusababisha ndoa kuvunjika ndani ya mwaka
1-2. Wanasema endapo watu waliooana wakianza kugombana kati ya mwezi wa
kwanza na kuendelea, basi ujue kuwa wanandoa hao hawawezi kuvuka miaka
miwili kabla ya ndoa yao kuvunjika.
Jambo
la kuzingatia katika sababu hiyo ya ugomvi iliyotajwa ni kwamba
watafiti hao hawachukulii hitilafu na migongano ya kawaida kama sababu, bali mikwaruzano mikubwa yenye kuumiza mwili au roho kwa kiasi kikubwa.
Watafiti
hao wanasema wanandoa wapenzi wanaogombana kwa kipindi hicho huwa na
kasoro ya ulinganifu wa tabia, mawazo na mwelekeo hivyo kuwafanya
wasiweze kuishi pamoja kwa muda mrefu.
Hivyo
ili wanandoa wasiweze kuachana katika miaka miwili ya mwanzo
wanashauriwa kuoana baada ya kuchunguzana vema tabia na kulingana katika
hali. (Soma TITANIC 1 njia za kuafuta mchumba)
Mwaka
mwingine wa hatari ni wa NNE. Baada ya kuoana mwaka wa nne unatajwa na
watafiti kuwa ni wa hatari katika kuwafikisha wapendanao ukingoni mwa
mapenzi yao. Sababu ambayo inapewa uzito katika kizuizi hiki cha ndoa ni kufanikiwa kupata MTOTO.
Kuwekwa kwa mtoto katika kizingiti hiki kunaonekana na tafiti nyingi
kuonesha kuwa wanandoa wanapofanikiwa kupata mtoto hujisahau na
kuhamisha mapenzi yao kwa mtoto, huku wakijisahau kuwa wao pia wana jukumu la kupendana.
Watafiti hao wanasema wapendanao wanapokuwa na mtoto, muda mwingi humfikiria zaidi yeye. Kama
ni suala la kuchukua zawadi za kurudi nazo nyumabani hazitakuwa kwa
ajili ya mume/mke bali itakuwa ni kwa mtoto. Pia msukumo wa kujali,
kuhudumia kubembeleza na ukaribu utahamia kwa mtoto, jambo ambalo
litawafanya wapendanao hao kujiona kama watu wasiohitajiana sana na hivyo kuleta hatari ya ndoa kufikia ukomo.
Ili
kukwepa ndoa kuvunjika katika mwaka huu, wanandoa wanashauriwa kuwa
baada ya kupata mtoto wasisahauliane, wawe na vipindi vya kuwa pamoja na
kushirikiana kama mwanzo, kwa lengo la kulinda upendo wao usiharibike.
Baada
ya kuvuka miaka hivyo, mwaka wa saba tangu kuoana unawekwa kuwa ni
mwaka wa kizingiti cha mwisho cha wanandoa kuachana. Kinachosababisha
hatari za mwaka huu kuwemo katika fungu hilo ni MAISHA, MAJUKUMU NA MAZOEA. Katika kufafanua mwaka huu watafiti hao wameeleza sababu nyingi, lakini za msingi ni hizo ambazo nimezitaja.
Wanasema
katika mapito ya maisha kuishi kwa wanandoa ndani ya ndoa kwa miaka
hiyo saba kutakuwa kumewatumbukiza katika kukabili matatizo mengi ya
kimaisha na hivyo kuwafanya wazidiwe na harakati za kujikimu. Kwanza watakuwa wamepata majukumu ya kulea familia, kutunza watoto wao, ambao tayari watakuwa wameanza kusoma n.k.
Lakini
sababu ya kuzoeana inatajwa kuchangia kuondoa msisimko wa kupendana na
hivyo kuamsha hisia potofu kuwa mwanandoa anaweza kuishi bila mume au
mke wake. Hivyo ili kulinda ndoa katika kipindi hiki cha miaka saba,
wanandoa wanashauriwa kutotumia muda wao mwingi kwenye pilika pilika za
kimaisha kiasi cha kukosa muda wa kuwa pamoja.
Hata
hivyo wakati watafiti hao wanakubaliana kuwa miaka iliyotajwa ni ya
hatari katika kuvunjika kwa ndoa, bado wanarudi katika kapu hilo kwa
kusema wanandoa ambao wanaachana baada ya kuishi kwa zaidi ya miaka hiyo
iliyotajwa, yaani miaka minane na kuendelea wanaingia katika kundi la
wazembe na wavivu wa kufikiria misingi ya ndoa yao.
Wanasaikolojia
wanasema watu walioishi kwa miaka hiyo huwa hawana majibu sahihi
yanayoweza kushibisha sababu za kuachana kwao. Wanachokiamini wataalamu
hao ni kuwa, hakuna tabia, mwenendo, migongano mabishano na purukushani
mpya za kimaisha zinazoweza kuwatokea wanandoa hao kiasi cha kuonekana
kuwa ni sababu za kupiku mazoea na kushindwa kuvumiliana.
Katika kuhitimisha hilo
niseme tu kwamba, ili kuepukana na kikwazo cha kwanza watarajiwa wa
ndoa wanashauriwa kuchanguana kwa kuzingatia ulinganifu wa tabia. Vijana
wengi siku hizi hawazingatii ulinganifu wa kitabia, badala yake
wanachagua wenza kwa kufuata uzuri na pesa, huku wakilenga kupata sifa
toka kwa rafiki zao
Katika
kikwazo cha pili, ushauri uliopo ni kuwa makini juu ya malezi ya watoto
na kuepuka kusahauliana. Watoto wanapaswa kuwa ndani ya upendo wa mume
na mke. Kuhusu kizingiti cha miaka saba, ushauri na kuepuka kuzoeana
na daima kujizatiti kukabiliana na changamoto za kimaisha bila kukata
tamaa.
No comments:
Post a Comment