PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Saturday, October 6, 2012

KIVUMBI KUTIMKA TENA LEO ENGLAND

  • Manchester city ikiwa nyumbani leo itakuwa na kibarua kigumu itakapo wavaa sunderland katika mchezo unaotegemewa kuwa mkali na wenye upinzani wa hali ya juu, hasa ikizingatiwa kuwa sunderland imekuwa na mwanzo mzuri msimu huu. Adam Johnson aliyekuwa mchezaji wa man city amehamia sunderland hivyo atakuwa na hamu ya kulipiza kisasi na kudhihirisha kuwa man city hawakuona uwezo wake. striker wa sunderland Steven Fletcher, ambaye yupo kwenye fomu nzuri sahv anatarajiwa kuipa wakati mgumu pia timu ya man city. tutegeme kuona mechi nzuri na yenye ladha.

    10/6/12 7:45 AM 
    Chelsea itakuwa na kibarua chepesi pale darajani hasa pale itakapo pambana na Norwich City ambayo haitarajiwi kuleta upinzani mkali dhidi ya chelsea ambayo ipo vizuri na imeanza vizuri msimu huu. itabidi Norwich ifanye jitihada zaidi ili kujiepusha na karamu ya magoli ambayo inaweza kuipa chelsea.
    -
  • 10/6/12 10:00 AM 
    -Swansea imekuwa ni timu inayocheza soka safi la chini lenye pasi nyingi zenye mvuto, itapambana na Reading ambayo imepanda daraja msimu huu, lakini bado haijawa na mwanzo mzuri katika ligi. Swansea wana nafasi nzuri yakushinda mchezo wa leo ambao watacheza wakiwa nyumbani.
  • 10/6/12 10:00 AM
    -Mechi ya West Bromwich Albion dhidi ya QPR itakuwa ngumu sana hasa upande wa QPR kwani wamefanya usajili mzuri msimu huu, liakini bado hawajapata matokeo mazuri, kitu ambacho kinamfanya kocha wa QPR  Mark Hughes awe na wakati mgumu wa kutafuta matokeo dhidi ya timu ambayo imeanza vizuri ligi msimu huu.
  • 10/6/12 10:00 AM
    -Wigan watakuwa na kibarua kigumu pale itakapo wakaribisha Everton ambao wapo kwenye kiwango cha hali ya juu msimu huu. hii itakuwa mechi yenye msisimko mkubwa na soka safi litapigwa.
  • 10/6/12 10:00 AM
    -Andy carrol anatarajiwa kuiongoza west ham dhidi ya Arsenal ambayo ipo vizuri sana msimu huu, hasa baada ya kufanya usajili mzuri ambao umedhihirika kuwa bora hasa pale wachezaji hao waliosajiliwa msimu huu kuonesha kiwango kizuri. hii pia itakuwa mechi nzuri yakuvutia.
  • 10/6/12 12:30 PM

No comments:

Post a Comment