PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Sunday, June 30, 2013

Tuzo tano zaenda brazili, Kipa bora na nyingine nne.


Bronze Boot : Neymar Jr.
Silver Boot : Fred
Golden Boot : Torres
______________________
Golden Gloves : Julio Cesar
_________________________
bronze ball : Paulinho
Silver Ball : Andres Ineista
Golden ball : Neymar Jr.





Brazil yamshushia Hispania kipigo cha mbwa mwizi





Timu ya Taifa ya Brazili imeendeleza rekodi yake yakutofungwa katika michuano ya Kombe la mabara iliyokuwa ikifanyika nchini humo, hasa baada yakuipiga bila huruma timu ya Hispania ambayo ndiyo timu iliyotwaa ubingwa wa ulaya na dunia.
Brazili walionekana kuutawala mpira kwa kiasi kikubwa, na kunako dakika ya pili ya mchezo huo brazili ilipata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake Fred. Karamu hiyo ya magoli iliendelea kunako dakika ya 44 kupitia kwa mshambuliaji hatari Neymar aliyefunga goli zuri kwa mguu wake wa kushoto.
Kunako dakika ya 46 mshambuliaji Fred aiipatia brazil bao la tatu.
Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa, Brazili wakawa wameibuka na ushindi huo mnono ambao umeharibu rekodi ya Hispania ya kutofungwa mechi 29.
Brazili imefanikiwa. Kutetea kombe hilo ililolichukua nchini Brazili ikiifunga timu ya USA katika mchezo wa fainali.

Wamachinga: ujio wa Obama nuksi kwetu



Dar es Salaam. Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara katikati ya jiji na kuondolewa kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama, wamelalamika kuwa sasa wanakabiliwa na maisha magumu.

Obama anatarajia kuwasili nchini kesho katika ziara ya kikazi ya siku mbili huku akiambatana na ujumbe wa watu wapatao 700.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabishara hao walisema kuondolewa huko kumewafanya kukosa kipato walichokuwa wakikipata hivyo kusababisha ugumu wa maisha.

Frank Mkama alilalamika: “Hapa Serikali isiseme kuwa wanafanya usafi wa jiji kwa kuwaondoa wafanyabiashara hii si kweli! Mbona hawakufanya zamani, hapa ni Obama ndiyo amesababisha sisi tukaondolewa.”

“Hivi sasa maisha yangu yamekuwa magumu. Kipato ambacho nilikuwa nakipata hapa na kula na familia yangu sasa sikipati.”

Naye, Elizabeth Makata alilalamika Serikali ilipaswa kuwaandaa wananchi kwa kuwaeleza ujio huo wa Obama watanufaika vipi na si kuwafanya waathirike kwa kuvunjiwa maeneo yao.

Alielezea wasiwasi kuwa huenda baada ya ziara hiyo wakashindwa kuendelea na biashara kwa kuwa watakuwa wamekula mitaji.

Kwa upande wake, Ramadhan Issa alisema ziara hiyo ya Rais Obama imeathri maisha yake kutokana na kuvunjiwa kibanda alichokuwa akifanyia biashara hivyo hajui hatima ya maisha yake.

Kadhalika askari polisi wakionekana kuongezeka katikati ya jiji wakipita huko na kule kuhakikisha hali ya usalama inaimarika.

Pia hali ya usafi imeendelea kuimarika kutokana na ujio kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa kwa lengo la kusafisha mazingira.

Licha kwamba wafanyabiashara hao wameondolewa hivi karibuni baadhi yao wameanza kurejea kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Thursday, June 27, 2013

CUF waahirisha maandamano yao



Dar es Salaaam. Chama cha Wananchi (CUF) kimeahirisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu kwa sababu Rais Jakaya Kikwete, atakuwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Smart Partnership na kushughulikia ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani.

Maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumfikishia Rais Kikwete ujumbe kuhusu vitendo vya ukatili, wizi, ubakaji na mauaji vinavyofanywa na polisi mkoani Mtwara na kutaka uchunguzi kuhusu matukio ya Arusha.

Hata hivyo kuahirishwa kwa maandamano hayo kunakuja baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote na kwamba polisi watapambana na yeyote atakayakaidi amri hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema: “Tumepokea barua kutoka Ikulu, kutuomba tusitishe maandamano hayo kwa sababu Rais ambaye ndiye mpokeaji wa maandamano hayo atapokea wageni mbalimbali watakaoingia nchini,” alidai.

Mtatiro alisema barua hiyo ilieleza kuwa haitawezekana Rais kupokea maandamano ya CUF kwa kuwa atakuwa akipokea wageni mbalimbali.

“Sisi tulimwandikia Rais barua kuwa Juni 29 mwaka huu tutakuwa na maandamano ya kuelekea Ikulu,hatukujua kama kutakuwa na ugeni wa marais siku hiyo...tumeahirisha,”alisema.

Obama kutunukiwa PHD Tanzania

Dar es Salaam. Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.
“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.
Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.
Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini Uingereza,David Mellor.

Wednesday, June 26, 2013

Marufuku kuja Dar wakati wa ziara ya Obama


Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.

Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.

“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.

Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.

“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”

Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.

 

Wasafiri wa mikoani

Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.

Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.

Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo.

Wengine watakaoathirika ni wakazi wa Kimara, Mbezi, Kibamba hadi Kiluvya. Athari nyingine ya usafiri itakuwa katikati ya jiji ambako Obama na msafara watakuwa na shughuli nyingi na hasa ile ya ufunguzi wa barabara karibu na Ikulu na kukutana na wafanyabiashara kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Jumatatu ijayo.

Watumiaji wengine wa barabara watakaopata shida ni wale wa Barabara ya Bagamoyo hasa pale Rais Obama na mkewe watakapokwenda kuweka mashada ya maua kwenye ubalozi wa zamani wa Marekani uliopuliwa na mabomu mwaka 1998.

 

Ulinzi hoteli za kitalii

Mashushushu wa ndani na nje ya nchi wamezingira kwenye hoteli kubwa za Dar es Salaam na walionekana katika baadhi ya hoteli hizo, wakiwatumia mbwa maalumu kufanya ukaguzi wa chumba hadi chumba.

Tofauti na utaratibu uliozoeleka, baadhi ya hoteli zenye hadhi ya nyota tano zimeanza kutumia mitambo maalumu ya kompyuta kuwafanyia ukaguzi wageni wote wanaoingia.

 

Wamchongea JK

Mtandao wa Kutetea Waandishi wa Habari Duniani (CPJ), umemwandikia barua Rais Obama ukimtaka kujadiliana kwa kina na mwenyeji wake Rais Kikwete wakati wa ziara yake nchini kuhusiana na vitendo vya kuuawa na kuteswa kwa waandishi wa habari wa Tanzania.

Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa CPJ, Joel Simon na nakala yake kusambazwa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete mwenyewe, mtandao huo ulitolea mfano wa kuuawa kwa Mwandishi wa Channel 10, Daudi Mwangozi na Issa Ngumba wa Redio Kwizera. Pia kupigwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda.

 

Marais waja Smart Partnership
Akizungumzia mkutano wa Smart Partnership utakaoanza kesho, Membe alisema utajadili jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia kukuza uchumi.

Viongozi watakaohudhuria mkutano huo ni Waziri Mkuu wa Malayasia, Najib Razak, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Uhuru Kenyetta (Kenya), Boni Yayi (Benin), Ali Omar Bongo (Gabon), Ikililou Dhoinine (Comoro), Faure Gnassingbe (Togo), Ernest Koroma (Sierra Leone), Blaise Compaore (Burkina Fasso), Mahinda Rajapaska (Sri Lanka) na Mfalme wa Swaziland, Mswati II, ambaye aliwasili jana.

Ujio wa Obama wasogeza ufunguzi wa sabasaba






Dar es Salaam. Ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya 37 ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (TanTrade), umesogezwa mbele kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Jackline Maleko, alisema maonyesho hayo yalitakiwa kufunguliwa Julai Mosi mwaka huu, lakini yamesogezwa mbele kupisha ujio wa Rais Obama na ule mkutano wa marais wa nchi wanachama wa Smart Patrnership.

Maleko alisema kutokana na hali hiyo, maonyesho hayo hayatafunguliwa siku hiyo, hadi wageni hao watakapoondoka nchini.

Alisema huenda yakafunguliwa kuanzia Julai 4 au 5, kulingana na ratiba itakayotolewa na Serikali.

“Ilikuwa tuzindue rasmi Julai Mosi, lakini tumebadilisha kutokana na ugeni wa viongozi hao, jambo ambalo mpaka sasa Serikali haijatoa taarifa rasmi ya tarehe maalumu ya ufunguzi huo,” alisema Maleko.

Maleko alisema kulingana na ratiba iliyopo, maonyesho hayo yatafunguliwa kama kawaida Juni 28, mwaka huu hadi Julai 8, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ndani na nje ya nchi.

Alisema kutokana na hali hiyo, wafanyabiashara wa ndani wanaweza kujenga mtandao wa biashara na wenzao wa nje, hiyo itawasaidia kupata masoko na kuongeza uzoefu.

Maleko alisema maonyesho ya mwaka huu, kutakuwa na bidhaa maalumu za ndani zitakazoonyeshwa kwa siku tofauti; asali, korosho na sanaa ya uchongaji.

Alisema lengo ni kutangaza soko la uzalishaji bidhaa hizo, jambo ambalo linaweza kuongeza masoko na kukuza mitaji kwa wazalishaji.

Pia, katika siku hizo, kutakuwa na siku maalumu ya kutangaza nembo ya Tanzania (Tanzania Brand) ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa sababu ndiyo muasisi wa siku nembo hiyo.Alisema tiketi za kuingilia kwenye maonyesho hayo zitaanza kuuzwa Juni 26.






Tuesday, June 25, 2013

Uchaguzi wa madiwani arusha bado kitendawili


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha tena uchaguzi katika kata nne za Jiji la Arusha, kwa sababu hali si shwari kuruhusu uchaguzi huru na wa haki.
Kata ambazo zilipaswa kufanya uchaguzi  Juni 30 ni Kimandolu, Elerai, Themi na Kaloleni ambazo uchaguzi wake uliahirishwa baada ya bomu kulipuka na kusababisha mauaji ya watu wanne na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mkutano wa mwisho wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Akizungumza, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba alisema: “Ni kweli tumeahirisha uchaguzi mdogo katika kata nne za Manispaa ya Arusha kwa kuwa hali bado si shwari kuruhusu uchaguzi huru na wa haki.”
Alipoulizwa kuhusu siku zilizoongezwa kama ndio kigezo cha kuwapo kwa hali ya utulivu na amani itakayoruhusu uchaguzi huru na wa haki kwa wananchi wa Arusha alisema: “Tunatumaini kuwa siku tulizoziongeza  hadi tarehe 14 Julai hali ya Arusha itakuwa imetulia.”
Aidha, katika kipindi chote hadi kufikia Juni 14, Tume ya Taifa imesema kampeni hazitaruhusiwa.
Tume ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza kurudiwa kwa uchaguzi mdogo katika kata nne za Arusha ambazo ni Kimandolu, Elerai, Themi na Kaloleni, ambazo zilisimamishwa kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani kutokana na vurugu zilizojitokeza katika kampeni za mwisho.
Akizungumzia uamuzi huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alisema: “Uamuzi huu ni mzito na wa majonzi, hata chama hakikufurahi kuufanya, ila kwa kuwa tunasimamia utashi wa chama, ikifikia hatua kama hii hatuna budi kuchukua hatua.”

Serikali yatoa ufafanuzi polisi kuua raia.



Yaeleza sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.

Dar es Salaam. Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.

“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.

Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.

Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.

Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.

Alieleza kuwa Kifungu cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.

Kauli hiyo ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi, ilitolewa ikiwa ni ufafanuzi wa jibu la swali la nyongeza lililoulizwa bungeni Mei 28,2013 na Rashir Ally Abdalah (Tumbe-CUF), ambapo Silima alisema mauaji yanayofanywa na askari polisi ni mauaji ya kisheria. Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashi Mohammed aliomba mwongozo wa spika kupata ufafanuzi wa kauli hiyo, na jana Silima kutoa kauli ya Serikali kujibu mwongozo huo.

“Ikumbukwe pia kuwa, kifungu cha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi Sura322, pamoja na Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi Na274, vinampa haki ya kisheria askari polisi kubeba na kutumia silaha za moto ikiwamo bunduki na mabomu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku..,”alisema Silima.

Alifafanua kwamba katika kutafsiri sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ikiwamo alizozitaja, mahakama katika nyakati tofauti imetoa msimamo wa kisheria juu ya suala hilo.

Akitoa mfano alisema: “Mathalan katika kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuri ya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa na Tanzania Law Report ukurasa wa 122, ambapo mshitakiwa (mwomba rufaa) alimjeruhi kwa panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwake na kuanza kumshambulia.”

Alisema katika kesi hiyo,mahakama ya rufaa pamoja na kuridhia uamuzi wa mahakama ya awali wa kumtia hatiani kwa kutumia nguvu kupita kiasi, ilibainisha kuwa mshtakiwa hakustahili adhabu kwani alitenda kosa lile wakati akijihami dhidi ya mashambulizi toka kwa mlalamikaji.

“Kwa msingi huo, tarehe 28 Mei, 2013 wakati nikijibu swali Na 290, nilitumia maneno ‘mauaji yanayofanywa kisheria’ nikimaanisha mauaji yanayotokea katika mazingira niliyoeleza..,”alisema Silima.

Hata hivyo alisema siyo nia ya Serikali kuhalalisha vitendo vya matumizi mabaya ya silaha ambavyo vinaweza kufanywa na askari wasio waadilifu.

Alibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kuheshimu haki za raia na kutumia busara kutatua migogoro.

Hata hivyo, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imelaani kauli ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi iliyoitoa jana na kueleza kuwa haikubaliani nayo kwa kuwa inatoa baraka kwa polisi kuendeleza mauaji ya raia.

Akizungumza na gazeti hili baada ya kikao cha bunge kuahirishwa, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa kambi hiyo rasmi, Vicent Nyerere alisema kauli hiyo ingekuwa na uthabiti kama askari polisi wangekuwa waadilifu.

“Kauli ingekuwa thabiti kama polisi wangekuwa waadilifu. kabla ya kutoa kauli hiyo, Serikali ilitakiwa kuchuja miongoni mwa askari wa jeshi la polisi, wa ngazi zote na kuwaondoa wasio waaadilifu ndipo wakatoa kauli hiyo wananchi wataielewa Serikali,”alisema Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini(Chadema).

Kwa upande wake, Mbunge wa Ole, (CUF) Rajab Mbarouk Mohammed akizungumzia kauli hiyo ya Serikali alisema kuwa majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima ni ya kisiasa.

Alisema kwamba kauli hiyo ni mwendelezo wa kauli iliyotolewa Alhamisi iliyopita na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwataka pilisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote watakaokaidi kutii sheria.

“Hakuna mwenye haki ya kuua, kuua ni kuua tu. Mahakama pekee ndiyo ina haki ya kuhukumu kifo baada ya kumtia hatiani mshtakiwa husika. Lakini kuwa polisi wanafundishwa utii, siyo kuua,”alisema Rajab.

Alifafanua kuwa kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao na kwamba kuruhusiwa kujihami haimaanishi kuua raia.

Nao Wabunge Aeshi Hilaly na Aly Keissy walisema ni vizuri raia wakatii mamlaka iliyopo na kutekeleza utii wa sheria bila shuruti.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu alisema: “Maoni yangu haki za watuhumiwa lazima ziheshimiwe.”

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS), Francis Stola alisema hakuna sheria inayompa mamlaka askari polisi kutumia nguvu za ziada ikiwemo kupiga raia pindi anapotekeleza majukumu yake,isipokuwa tu anaweza kutumia nguvu kiasi iwapo raia anayekabiliana naye anaonyesha vitendo vya kukaidi amri ama kuhatarisha usalama.

Stola ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kauli bungeni alisema kuwa kwa kufuata sheria polisi haruhusiwi kupiga raia. “ Ukisoma sheria hakuna mahala utakuta kuna neno limeandika piga…. Askari polisi anachoweza kufanya ni arrest(kamata) na siyo vinginevyo, hana mamlaka kabisa ya kupiga raia”

Alisema sheria imetamka wazi kuwa kunapojitokeza hali yoyote inayopaswa kdhibitiwa na vikosi vya ulinzi, nguvu inayopaswa kutumika ni ile ya kawaida na kwamba kitendo cha kutumia risasi za moto ama kupiga raia ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

Alisema polisi anapaswa kutoa mwongozo kwa raia kumwelekeza jambo la kufanya iwapo kunajitokeza hali ya sintofahamu,lakini hapaswi kutumia nguvu kupita kiasi ikiwemo kuwapiga raia

“ Sheria inasema wazi kwamba panapojitokeza hali yoyote korofi, polisi wanatakiwa kutumia nguvu ya kawaida tu kukabiliana na hali hiyo na wala siyo kutumia silaha za moto… silaha za moto zinaweza kutumika tu iwapo kunajitokeza tukio ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa maisha ama mali isipotee” alisema

Kuhusu wananchi kufanya maandamano, rais huyo alisema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia,lakini yanafanyika katika utaratibu maalumu. “ maandamano ni haki ya kila raia lakini panapaswa kuwa na utaratibu maalumu…. Kama kunajitokeza maandamano ambayo hayana utaratibu polisi wanapaswa kutumia reasonable force (nguvu ya kawaida) kudhibiti maandamano hayo na wala siyo kutumia nguvu za ziada.

Furahia Maisha: DALILI ZA NDOA INAYOKUFA

Furahia Maisha: DALILI ZA NDOA INAYOKUFA: DALILI ZA NDOA INAYOKUFA Jitahidi kuhakikisha unalinda moyo wako na moyo wa mpenzi wako; usije ukaupasua na kuuumiza. Wanandoa weng...

DALILI ZA NDOA INAYOKUFA


DALILI ZA NDOA INAYOKUFA


Jitahidi kuhakikisha unalinda moyo wako na moyo wa mpenzi wako; usije ukaupasua na kuuumiza.
Wanandoa wengi hujikuta wamefika mahali ambapo ndoa haiwezi kuwepo tena (talaka) na tatizo kubwa ni kwamba wengi hukaa bila kuchukua hatua zinazostahili (serious) wakati tatizo au mgogoro unapojitokeza ili kumaliza tatizo
Kutoshughulikia vizuri tatizo lolote kwenye ndoa hupelekea Chuki, Uchungu, Kinyongo, Kuumia hisia na huweza kusababisha mwanandoa mmoja kujiondoa katika muungano wa kindoa uliopo (kuanza kuishi kivyake katika kufikiria na kutenda).

 Zifuatazo ni dalili mbaya sana ambazo zinaonesha ndoa inayoelekea kwenye kifo

 KUFIKIRIA MAISHA KIVYAKO BILA MKE AU MUME KUMUHUSISHA
Ukiona unaanza kufikiria uzuri wa maisha utakavyokuwa bila mwenzi wako kwa maana kwamba kuwa na yeye unaona asilimia mia moja anakulostisha, au hana maana kabisa ni dalili kwamba hiyo ndoa inaelekea kwenye kifo cha ghafla. Na kama unasongwa sana na mawazo kutaka kuishi mwenye au na mtu mwingine zaidi ya huyo uliye naye na kujiona utakuwa na amani zaidi basi unaelekea kubaya kwani inaonesha umeshapoteza nafasi yake ndani ya moyo wako na kitu cha msingi waone washauri wa mambo ya ndoa ili waweze kukusaidia.
 MAMBO MABAYA NI MENGI KULIKO MAMBO MAZURI KWENYE NDOA YAKO
Kama mnajikuta ndoa yenu ina mambo mabaya mengi zaidi kama vile kutokuelewana, kila mtu ana hasira, mnapishana lugha kila mara, hakuna kucheka wala kufurahishana na mambo mazuri kama kucheka pamoja, kufurahi pamoja, kujisikia bila mwenzako siku haiendi basi hiyo ni dalili kwamba hiyo ndoa inahitaji msaada na bila kuifanyia ukarabati basi itasombwa na mafuriko na hatimaye kufa.
 UNAJISIKIA VIGUMU SANA KUWASILIANA NA MKE AU MUME WAKO
Je, unajisikia kupatwa na hofu au mashaka kuongea na mke au mume wako kuhusu matatizo ya ndoa yako au maisha yenu kwa ujumla? Mawasiliano ndiyo njia pekee ya kuondoa stress za ndoa na maisha kwa ujumla na hatimaye kujenga ndoa yenye afya kwa wanandoa. Kama mkiwa pamoja mnakuwa kimya bila kuongea chochote na hakuna dalili ya kutaka kuongea na mwenzako basi kuna tatizo kubwa sana, hasa kama ni tofauti sana na kawaida yenu hasa jinsi ilivyokuwa katika siku za kwanza wakati mnachumbiana. Kama hujisikii vizuri kuwasiliana na mwanandoa mwenzio basi hiyo ni dalili kwamba tayari umekosa imani kwake na ndoa huwa inakuwa katika wakati mgumu kukiwa kauna kuaminiana (trust) Pia kama wewe ni mtu wa mwisho kujua kitu chochote muhimu au kuzuri kuhusu yeye, basi hapo kuna tatizo kwani ni kawaida wanandoa kuelezana vitu vizuri vinavyotokea kwa mmoja wao.
 KILA MMOJA KUKATAA KUHUSIKA NA MATATIZO AU MIGOGORO YA NDOA INAPOJITOKEZA
Kama kila mmoja anajilinda na kutothamini hisia za mwenzake hasa linapotokea tatizo na kuanza kumrushia mwenzake lawana kwamba ndiye muhusika na wote mnakuwa na msimamo huohuo, fahamu kwamba hapo ndoa inapitiliza hata tiba za uangalifu zinazopatikana ICU. Ikiwa migogoro au matatizo yanapojitokeza kuna kuwa na kushindana kwa kila mmoja kukwepa kuhusika na badala ya kupata suluhisho mnajikuta mgogoro unazidi kuongezeka basi hiyo ni dalili kwamba sasa mmeanza kubusu kifo cha ndoa.
 KUJIKUTA NI WEWE PEKE YAKO TU UNAHUSIKA KATIKA KUTATUA MIGOGORO AU MATATIZO YA NDOA.
Je, umekata tamaa, au kujisikia vibaya kuongea masuala ya matatizo ya ndoa yako kwa sababu mwenzako anakurudisha nyumba, au imefika mahali na wewe umeamua kunyamaza na kuachana kabisa na kujishughulisha na tatizo lolote katika ndoa na matokeo yake hakuna hata mmoja anajali tena kushungulikia matatizo ya ndoa? Kama mpo kwenye matatizo na kila mmoja amenyamaza kimya katika kuhakikisha mnamaliza tatizo lililopo basi hii ndoa ipo ICU na kama mtabaki kimya bila kila mmoja wenu kuhusika ili kuhakikisha ndoa inarudi kwenye mstari basi ni kama bomu lililotegwa ardhini na siku mtu akikanyaga hakuna kitakachosalia.
 TENDO LA NDOA
Kama mmoja wenu sasa hana hamu kabisa na tendo la ndoa, au wote kwa pamoja hamna hamu kabisa ya tendo la ndoa hiyo ni dalili kwamba somethings is wrong. Kukosa faragha ya pamoja (intimacy and affection) itawafikisha mahali ambapo ndoa inaweza kufa au kuwa na ndoa isiyokidhi haja au kukosa kuridhishana inavyotakiwa.
Je mnaishi tu kwa sababu ya watoto ndo wamewafanya msiachane?
Kama ni ndiyo basi mnahitaji kupata msaada wa washauri wa mambo ya ndoa kwani hakuna tatizo lolote kwenye ndoa ambalo halina jibu. Kama hakuna hamu ya mapenzi kwa mmoja wenu au wote maana yake hisia zenu zipo mbali sana na hiyo ni dalili kwamba kila mmoja anaenda njia yake.
 KUBISHANA AU KUGOMBANA KWA KITU KILEKILE KILA MARA
Kama kubishana, kupishana, kugombana, kuanzisha zogo kila mara kunatokana na issue ileile moja bila kupata suluhisho basi hiyo ndoa imesimama haikui wala kuelekea kwenye uimara zaidi bali inatelemka kwenda kwenye shimo. Kamahakuna kitu kipya kinatokea ili kupata ufumbuzi wa hiyo hali basi tafuta mshauri wa mambo ya ndoa ili awasaidie.
HITIMISHO
Hakuna tatizo la ndoa ambalo halina jibu hapa duniani kuna washauri wa mambo ya mahusiano na ndoa, wazazi ambao hupenda mafanikio ya watoto wao, kuna wachungaji ambao wana hekima na busara walizopewa na Mungu kwa ajili ya kuwashauri hivyo hata kama kuna tatizo kubwa namna gani jibu lipo na tiba ipo. Anza kwa kuzungumza na mwanandoa mwenzako then ikishindikana nenda kwa watu mnaona wanaweza kuwasaidia, usiwe mbishi wala mbabe ndoa ni kuchukuliana na kuelewana.

Furahia Maisha: MAMBO 6 YAKUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI...

Furahia Maisha: MAMBO 6 YAKUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI...: Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu.    Wanawak...

MAMBO 6 YAKUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI


Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu.  Wanawake wengi wanalalamika kuwa  hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.
Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika,  muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala.  Wengi walioachana au kutalikiana nao  walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.
Njia za kukusaidia
1.       kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote.  Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu.  Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea.  Kama utaanza kujizoeza  hivi ukiwa nyumbani, taratibu  utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.

2.       Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake.  Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo.  Onyesha heshima katika vitu hivyo pia.  Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu.  Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.  Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo.  Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua  na sisi pia.

3.       Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote.  Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.  Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili.   Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au  dhambi?
Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa  tendo la ndoa katika  mahusiano yenu.
4.       Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano.  Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao.  Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu.  Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu.  Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu.  Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.
5.       Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu.  Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia.  Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu.  Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu.  Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.
6.       Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko.  Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano  wetu lazima ume halisi na sio feki.  Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi.  Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu.  Ukianza kupata  ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe kuvitafuta vile vyote  mpenzi wako alivyonavyo ambavyo  hukuza ukaribu wenu.  Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.

Gharama za simu kupanda Julai


GHARAZA za huduma za simu kwa mtumiaji zinatarajiwa kuongezeka kuanzia Julai mosi mwaka huu.
Ongezeko hilo limetokana na serikali kuongeza kodi katika huduma za simu za mkononi.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania (MOAT) imesema pendekezo la serikali kutoza kodi kwa asilimia 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi haliwezi kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.
Kwa mujibu wa MOAT, awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwamba ongezeko la kufikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.
“Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha huduma za mawasiliano kuwa ni huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na kampuni za mawasiliano ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia,” inaeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Kampuni za Simu za Mkononi za Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel.
Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti katika Bara la Afrika, ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40.
MOAT ilisema mawasiliano ya simu si anasa, bali ni huduma muhimu katika Tanzania ya leo, sasa inakuwaje kuwatoza kodi mara kwa mara watu hao hao ambao wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao?

Atakayefichua wakwepa kodi kupewa gari au fedha.


SERIKALI imeamua kutoa zawadi ya gari na fedha kwa mtu yeyote atakayeongoza kudai risiti za bidhaa au huduma atakayopatiwa.
Uamuzi huo wa serikali umelenga kuwabana wafanyabiashara na watoa huduma wanaokwepa kulipa kodi za serikali.
Akitangaza uamuzi huo jana bungeni, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya, alisema wananchi watapaswa kuwataja wafanyabiashara watakaokataa kuwapa risiti hizo baada ya kuwauzia bidhaa.

Mkuya pia alitangaza namba za simu ambazo wananchi watapiga bure na kuwaomba wabunge wasaidie kuwaarifu wananchi kuhusu namba hizo ambazo ni 0800110016 kwa watumiaji wa Voda na TTCL, Airtel 0786800000 na Tigo 0713800333.
Alisema kuwa namba hizo watazibandika maeneo mbalimbali na kuzitangaza kwenye vyombo vya habari na kila mwananchi atakayechukua risiti ya malipo ya bidhaa au huduma ataingizwa kwenye utaratibu wa kupata zawadi.

Mkuya alifafanua kuwa utaratibu wa kutoa zawadi kwa washindi utafanyika kila wiki, mwezi na baadaye kwa mwaka ambapo zawadi hizo ni pamoja na gari na fedha taslimu.
Utaratibu huu utaanza Julai mosi, hivyo akawataka wananchi kuhamasika kudai risiti kila wanaponunua bidhaa, vile ile wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kutoa risiti hizo.
Kuhusu mashirika kuorodheshwa kwenye Soko la Mitaji na Hisa la Dar es Salaam (DSC), alisema kuwa lazima liwe na vigezo kama vile historia nzuri ya utendaji na kutengeneza faida kwa miaka isiyopungua mitatu kwa sababu lengo lao ni kuongeza mtaji.
Aliongeza kuwa shirika au kampuni inapaswa kufanya maombi ya hiari ndipo isajiliwe baada ya kutimiza masharti hayo.
Alizitaja baadhi ya kampuni na taasisi zilizomo DSE kuwa ni Benki ya NMB, TOL, TCC, CRDB, TBL, Swissport, Twiga na Tanga Cement.
Aliyataja mashirika mengine ambayo yako kwenye mchakato wa kuingia hivi karibuni kuwa ni Mtibwa Sukari, Kilombero Sukari, Mbeya Sementi, Tanalec, Alaf, NBC na Airtel.

Meno ya Tembo yenye thamani ya sh milioni 200 yakamatwa mkoani Ruvuma

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na maofisa Wanyamapori katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma limekamata meno ya tembo 18 yenye thamani ya sh milioni 216.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, alisema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Nsimeki alisema kuwa tukio hilo limetokea Juni 20, mwaka huu majira ya saa tisa usiku nje kidogo ya Kijiji cha Majala, Kata ya Nandepo, katika Wilaya ya Tunduru, ambapo askari polisi wakiwa doria waliwaona watu wanne wakisukuma baiskeli zao kuelekea katika kijiji hicho.
Kamanda Nsimeki alisema watu hao walipoona mwanga wa taa za gari la polisi walishtuka na kuzitupa baiskeli zao nne zilizokuwa zimebeba vifurushi na kukimbia.

Alisema askari walipofika eneo zilipotupwa baiskeli hizo na mizigo yake waligundua kuwa ni meno ya tembo 18 yenye uzito wa kilo 84, ambazo zinakadiriwa kuwa na thamani ya sh milioni 216.
Kamanda Nsimeki alisema jeshi hilo mpaka sasa halimshikilii mtu yeyote kuhusu sakata hilo lakini linaendelea na jitihada za kuwatafuta waliozitelekeza baiskeli hizo.
Alisema katika kipindi hiki kifupi polisi wamekamata meno ya tembo kwa wingi na tukio hili ni la tano na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa taarifa za siri kwa jeshi hilo.

Aliongeza kusema kuwa mafanikio hayo ya kuwakamata waalifu pamoja na majangili mkoani humo kunatokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na watendaji wa jeshi hilo.
Kamanda Nsimeki alisema vita ya kupambana na wawindaji na wafanyabiashara ya meno ya tembo au rasilimali nyingine za taifa zinahitaji ushirikiano wa kila mwananchi.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Songea wameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa zawadi kwa wasamaria wema wanaotoa taarifa sahihi za kuwafichua watu wanaojihusisha na biashara ya meno ya tembo.

Watuhumiwa wa bomu arusha waachiwa

WATU watatu waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za urushaji bomu katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa CHADEMA, Juni 15 eneo la Soweto wameachiwa.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi juu ya suala hilo ukiwa bado unaendelea.
Alipotakiwa kuwataja watuhumiwa hao, Kamanda Sabas hakuwa tayari kwa kusema ni mapema mno kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa sababu uchunguzi wa suala hilo unaendelea.
Alifafanua kuwa watuhumiwa walihojiwa na askari wa upelelezi kuangalia uhusiano wao na mlipuko wa bomu katika viwanja vya Soweto na baada ya kukamilika mahojiano hayo wameachiwa kwa dhamana.
Alisema kuwa jeshi hilo halihusiki na mpango wa kutaka kutorosha majeruhi walioko hospitali walioeleza tukio hilo na kudai ni taarifa za mitaani .
“Kuhusu propoganda zilizoenea jijini Arusha kuwa vyombo vya dola vina mpango wa kutorosha wagonjwa wanaosema ukweli hospitalini na kuwapeleka kusikojulikana si za kweli na ni upotoshaji,” alisema.
Alisema polisi au watu wa usalama wana wajibu wa kuhoji mtu yeyote pale tukio linapotokea ili kubaini ukweli wa jambo, hivyo wagonjwa hao hawana haja ya kuogopa na wasitishwe na maneno ya uongo ya mitani.
Sabas alisema hivi sasa wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Freeman Mbowe, pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wabunge wanne wengine na wafuasi wao 70.

Monday, June 24, 2013

Marekani yatoa onyo kali kwa msafara wa Rais Obama Dar




Dar es Salaam. Licha ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.
Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.
Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi
Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa na gharama kwa walinzi, lakini safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.


Bajeti ya serikali yaridhiwa Bungeni

Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2013/14, Dodoma jana.

 Dodoma/Dar. Bunge limepitisha Bajeti ya Serikali ya Sh18.2 trilioni iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa katika Bunge la Bajeti linaloisha mwishoni mwa wiki hii.
Wabunge 235 walipiga kura ya ndiyo kupitisha bajeti hiyo jana jioni baada ya Dk Mgimwa na manaibu wake wawili kumaliza kujibu hoja mbalimbali za wabunge kuhusu bajeti hiyo.
Akitaja majibu ya kura zilizopigwa kupitisha bajeti hiyo, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema wabunge wote wako 354 kati ya hao wabunge 83 hawakuwepo na kwamba waliopiga kura ni wabunge 270. Alisema 35 walisema hapana na 235 walisema ndiyo.
“Kwa mujibu wa kanuni zetu wabunge waliosema ndiyo wamezidi asilimia 50 ya adadi inayohitajika hivyo bajeti kuu imepitishwa rasmi,” alisema Joel.
Kati ya wabunge 83 ambao hawakuwepo wakati wa zoezi hilo la kupiga kura likifanyika wapo mawaziri sita.
Mbunge wa Bariadi Mashariki(UDP), John Cheyo alipiga kura ya ndiyo na kufanya wabunge wa CCM wamshangilie kwa kufanya hivyo.
Kwa upande mwingine, wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, jana walisusia kikao cha Bunge cha kupitisha Bajeti ya Kuu, huku wakitoa sababu tano, ikiwemo shambulio la bomu katika mkutano wa chama hicho jijini Arusha.
Mbali na kususia kikao hicho, jana asubuhi Kiongozi wa Kambi hiyo, Freeman Mbowe, Mnadhimu Mkuu, Tundu Lissu, Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje walizuiwa kuingia katika Ukumbi wa Bunge kwa maelezo kuwa wamevaa kombati (sare zinazotumiwa na chama hicho).
Tangu Juni 17 mwaka huu wabunge wa chama hicho hawakuhudhuria mjadala wa bajeti, badala yake walikwenda kushiriki shughuli za mazishi ya watu waliokufa baada ya kutokea kwa mlipuko wa bomu wakati chama hicho kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Kambi ya Upinzani Bungeni, Lissu ambaye alitumia dakika 36 kufafanua sababu za kutoshiriki kwa chama hicho.
“Hatukushiriki kwa sababu ya matukio yaliyotokea baada ya shambulio la bomu na kauli zilizotolewa ndani na nje ya Bunge,” alisema.
“Uamuzi huo umekuja baada ya wabunge wote wa chama hiki kukutana jana kwa saa 3, kujadili jinsi ya kushiriki katika mjadala wa kuhitimisha bajeti hiyo.”