PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Monday, September 30, 2013

JE, UNAUFAHAMU UGONJWA WA KISUKARI?

Kisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini.

Aina za Kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo;
1. Aina ya kwanza ya Kisukari au Type 1 Diabetes Mellitus
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana (young adults).
Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans katika tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

2. Aina ya pili ya Kisukari au type 2 Diabetes Mellitus
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.
Hali hii husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa (physical inactivity).
Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake, wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)

3. Kisukari cha Ujauzito (Gestational DM)
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito. Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2-5 ya mama wajawazito wote ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua.

Viashiria vya ugonjwa wa kisukari (risk factors)
• Unene uliozidi na kiribatumbo
• Ulaji mbaya wa chakula
• Baadhi ya madawa
• Msongo wa mawazo
• Historia ya ugonjwa wa kisukari kwenye familia
• Tezi ya shingo (husababisha mwili kukua na kuongezeka haraka)
• Kutofanya mazoezi
• Umri zaidi ya miaka arobaini (kadri tunavyozeeka na kongosho letu linapungua uwezo wa kutoa insulin hivyo kusababisha kisukari)
• Magonjwa yanayoharibu kongosho
• Akina mama wanaojifungua watoto wenye kilo zaidi ya arobaini (Mara nyingi hawa akina mama huwa na ugonjwa wa kisukari ila hawagunduliki hadi mtoto anapozaliwa na kuonekana mkubwa)
• Akina mama wenye historia ya kisukari wakati wa ujauzito
• Utumiaji uliozidia pombe na uvutaji sigara

Dalili za ugonjwa wa kisukari
• Kiu ya mara kwa mara
• Kupungua uzito licha ya kula vizuri
• Njaa kali na ya mara kwa mara
• Jasho jingi
• Uchovu usioeleweka hata bila kufanya kazi
• Kizunguzungu
• Macho kupungua uwezo wa kuona
• Kidonda kisichopona haraka

No comments:

Post a Comment