PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Afya


MAGONJWA 24, YANAYOAMINIKA KUTIBIKA/KUTULIZWA NA KITUNGU SWAUMU:

1.Kiua sumu mwilini
2.Kisafisha tumbo
3. Kiyeyusha mafuta(cholestro)
4. Kusafisha njia ya mkojo
5. Kutibu amoeba
6. Kuzuia kuhara damu(Dysentery)
7. Gesi tumboni
8.Msokoto wa tumbo
9.Typhoid
10.Mabaka kwenye ngozi
11. Mafua
12.Kifua kikuu cha mapafu
13.Kipindupindu
14.Kutoa minyoo
15.Upele
16.Kuvunjavunja mawe katika figo
17.Mba kichwani
18.Kuupa nguvu ubongo
19.Kuzuia meno kung'ooka na kutuliza maumivu
20.Nguvu za kiume
21.Maumivu ya kichwa
22. Kizunguzungu/kisunzi
23. Shinikizo la damu
24. Saratani (cancer)

Pia jitahidi kula japo punje moja ya Kitungu swaumu kwa siku, hukukinga na magonjwa mengi.




FAHAMU VYAKULA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME


Ukweli ni kwamba ndoa nyingi za Kikristo zinavunjika kutokana na tatizo hili. Je, hakuna haja ya kuitisha mjadala wa kitaifa? Taifa letu linaangamia kwa kukosa maarifa.

Hivi upungufu wa nguvu za kiume ni nini? Kifupi ni mwanamume kutokuwa na uwezo wa kutoa mbegu bora zenye uwezo wa kutungisha mimba, au kutosimama kwa uume.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya wanandoa nchini wanakabiliwa tatizo hili. Kwa hiyo, mabango ya waganga yaliyopo barabarani hayajapunguza kabisa tatizo hilo.

Hawa watu wanatibu watu au majini? Hapo ndipo kiini cha makala haya. Sababu kubwa ya ongezeko la wenye matatizo haya ni kwamba dawa nyingi zinazodaiwa kuponya tatizo hili hazina viwango vya kuitwa dawa, bali ni vichocheo tu kwani kinachopigiwa chapuo huwa ni kumudu tendo kitandani na si nguvu asilia.

Waganga wengi wameelekeza nguvu zao huko na ni hapo ndipo janga hili la kitaifa linapoota mizizi.

Ukweli ni kwamba upungufu wa nguvu za kiume hauondolewi kwa dawa za kuchochea nguvu wakati wa tendo. Hizi zina madhara makubwa na mara kadhaa husababisha vifo kwa wanamume wengi wakiwa ‘guest’ na vimada wao kwani hulipua moyo.

Ni lazima kiini cha tatizo hili kichunguzwe na tiba stahiki ipatikane. Kinyume cha hapo, janga hili linaweza kugeuka na kuwa dubwana kubwa la kutumaliza.

Matatizo ya nguvu za kiume huchangiwa na kuugua kwa muda mrefu, ugonjwa wa kisukari, kuvaa nguo za kubana sana, mionzi ya simu, kompyuta na mengineyo. Pia dawa za kuua wadudu huleta tatizo hili kwani zina viambata sumu viitwavyo ‘estrogen’, matatizo ya kisaikolojia, kupiga punyeto kwa muda mrefu na kutumia vyakula vyenye kemikali.

Utafiti unasema kuna uhusiano mkubwa sana kati ya upungufu wa nguvu za kiume na kuwa na sumu mwilini zinazotokana na vyakula vyenye kemikali tunavyobugia kwa kupenda au kutokupenda.

Ni kutokana na utafiti huo ndipo dawa bora yenye uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini kwa muda mfupi ikagunduliwa. Hii ikiwekwa kwenye kinywaji chochote chenye kemikali, mara moja hutenganisha sumu iliyomo humo.

Dawa hii pia huleta nguvu za kudumu za kiume, hujenga afya na kuleta nguvu asilia. Hutatua tatizo la nguvu za kiume huku ukiondoa pia tatizo la ugumba na ni vizuri wenye matatizo kama hayo wakatumia vyakula vya protini hasa ya mimea kwani hurutubisha mbegu.

Kuna aina 2 ya vyakula ambavyo vimefanyiwa utafiti na kubaini kuwa ni moja ya vyakula vinavyosaidia kuongeza nguvu za kiume na havina madhara katika engezeko la nguvu za kiume, katika vyakula hivyo vyenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kiasili ni:

1. TANGAWIZI
- Tangawizi ni moja ya chakula kinachoweza kurejesha nguvu za kiume, unaweza kuichemsha tangawizi na ukatumia kwa kuinywa kama chai Asubuhi, mchana na jioni pia Tangawizi unaweza ukaitumia katika mchanganyiko wa kiasili kwa kutumia habat soda,asali,kitunguu saumu na tangawizi yenyewe. JINSI YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU: Chukua tangawizi na kitunguu saumu vitwange kisha vichanganye na asali pamoja na unga wa habat soda na uwe unakunywa mchanganyiko huu kwa kutumia kijiko cha chai kimoja kutwa mara 3 kwa muda wa wiki moja na utaona mabadiliko.

2. TIKITI MAJI:
-Chakula kingine kinachosaidia katika upande wa kuongeza nguvu za kiume ni tunda la Tikiti Maji, unaweza ukachukua tikiti lako ukalikata na kutengeneza juice ya Tikiti kisha unakunywa ila sio lazima utengeneze Juice hata lenyewe tu unaweza ukalila. Ila jitahidi kutumia tunda hili hata kila siku kwani linasaidia sana kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.




Baadhi nya madhara ya utumiaji wa vipodozi vyeme kemikali 

Utafiti wa Profesa Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Georgia, Atlanta, Marekani, Kelly Lewis wa kitengo cha Sosholojia, kuhusu wanawake wanaotumia ‘mkorogo’ Tanzania umebainisha 
Wanawake zaidi ya 6milioni nchini huenda wakaugua saratani, kuzaa watoto wenye mtindo wa ubongo au kupoteza maisha kutokana na kukithiri kwa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatari.

Utafiti wa Profesa Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Georgia, Atlanta, Marekani, Kelly Lewis wa kitengo cha Sosholojia, kuhusu wanawake wanaotumia ‘mkorogo’ Tanzania umebainisha hayo.

Taarifa ya utafiti huo inaonyesha kuwa asilimia 30 ya wanawake, sawa na 6 milioni ya wanawake wote nchini ambao ni milioni 23, wanatumia vipodozi vyenye kemikali hatari, vyenye madini ya zebaki, hydroquinone na maji ya betri.

Dk Lewis akishirikiana na timu ya Watanzania 20, aliwahoji wanawake 420 katika Jiji la Dar es Salaam ambapo wengi walikiri kujichubua kwa sababu ya dhana kuwa weupe ni uzuri, pamoja na kuwaridhisha wenza wao wanaopenda wanawake weupe.

Utafiti huo wa Shahada ya Uzamivu ulifanyika kuanzia mwaka 2000 na kumalizika Mei 17, 2012.

Profesa Lewis anasema kuwa vipodozi hivyo hasa vyenye madini ya zebaki, kwa kiasi kikubwa husababisha ugumba, saratani na maradhi ya figo.
“Inatisha.

Wanawake hawatumii ‘mikorogo’ ya dukani pekee, lakini pia wanatengeneza mikorogo ya kijadi kwa kuchanganya asidi ya maji ya betri ya gari, dawa ya meno na sabuni ya unga,” anasema Dk Kelly.Akizungumza kwa njia ya Barua Pepe, Profesa Lewis anasema kuwa anatarajia kufanya kipindi kuhusu wanawake wanaotumia mikorogo Tanzania ili kutoa elimu.

‘Kutokana na maombi mengi, nimefungua Kituo cha Utalii kwa Umma na nitafanya safari mbili za kuja nchini Tanzania,” anasema.

TFDA imebainisha vipodozi vyenye sumu kuwa ni pamoja na ni Carolight, inayotajwa kuwa na sumu kali zaidi pamoja na vile vyenye madini ya zebaki au mercury, ikiwamo sabuni ya Jaribu na Mekako.

Vipodozi vingine ni vile vilivyochanganywa na viambata sumu kama Clobetasol na Betamethasone ambapo itajwa pia krimu ya Amira, Betasol na Skin Success.

Inaelezwa kuwa wanawake wanaotumia mafuta ya aina hiyo wakiwa wajawazito huwaathiri watoto walioko tumboni.

Asilimia 70 ya vipodozi hivyo hutoka nje ya nchi, ambapo imebainika kuwa hakuna sheria kali za udhibiti wa dawa na vipodozi.                               

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza kuwa asilimia 10 ya dawa duniani kote ni bandia au duni.

Taarifa zaidi zinasema kuwa zaidi ya asilimia 50 ya dawa bandia zinatengenezwa kutoka katika maabara za chini ya ardhi zilizopo China na India.

Dawa bandia ni zile ambazo mtengenezaji amebadili viambata, nembo, vifungashio au amedanganya kwa namna yeyote kwa lengo la kujipatia kipato.
Dawa duni ni zile ambazo mchanganyiko wa viambata vyake haukidhi viwango vya ubora vinavyokubalika kisayansi.

Dawa bandia zilizokamatwa na TFDA
Mkurugenzi wa Shirika la Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Paul Sonda, anasema kuwa Agosti 2011 dawa ya Malaria aina ya Laefin, ilitengenezwa na kusambazwa katika mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora, Shinyanga na Kagera.

Dawa hiyo ilighushiwa kwa teknolojia ya hali ya juu.Watengenezaji hao waliweza kunakili kila kitu kasoro herufi moja katika jina, ambapo badala ya kuandika Laefin waliandika ‘Laifin’ wDawa nyingine ya Malaria, aina ya Coartem ilitengenezwa na kusambazwa madukani na dawa halisi ilitakiwa kutumika kuanzia Machi, 2007 na kwisha muda wake Februari 2009.

“Baada ya kwisha muda wake, wajanja walibadili muda na kuandika imetengenezwa Machi 2009 na muda wake utakwisha Februari, 2012,” anasema.

Dawa hiyo ilisambazwa zaidi katika Wilaya za Kilombero na Ulanga Morogoro kuanzia Agosti na Septemba 2011.

Ibrufen
Sonda anasema kuwa dawa ya maumivu ya Ibuprofen iliuzwa kama Erythromycin (antibiotic inayotibu magonjwa ya kuambukiza)
Kwa kuwa Ibuprofen na Erythromycin zinafanana kwa rangi na kwa umbo, wajanja walitumia mfanano huo na kuziweka katika mfumo wa soko.

Dawa hizo zilipatikana katika mikoa ya Ruvuma katika Hospitali ya Litembo

Wilaya ya Mbinga
Eloquine
Sonda anaongeza kuwa pia mwezi Februari mwaka 2011, dawa ya malaria aina ya Eloquine au Kwinini Sulphate ilighushiwa na iligundulika katika maeneo ya Moshi, Kilombero na Ulanga.

Sonda anasema kuwa TFDA ilibaini kuwa vidonge vya Eloquine havikuwa na kiambata cha ‘Quinine Sulphate’ badala yake uchunguzi ulibaini kuwa ni dawa ya kuzuia kuharisha aina ya Flagyl au Metronidazole.

Dawa aina ya Pen V, ilitengenezwa na kile kinachodaiwa kuwa ni unga wa ngano.

Pen V hutumika kutibu maradhi ya kuambukiza, vidonda. (Antibiotic) Wakaguzi walipoikagua waligundua kuwa dawa hiyo inaganda ndani ya kopo pindi unapoliinamisha.

Bidhaa zinazosadikiwa kukuza maumbile(hip lift up na hip massage cream), nazo zilipigwa marufuku ingawa bado zinauzwa kwa njia ya panya katika maduka.

Mkurugenzi huyo wa TFDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini anasema kuwa thamani ya dawa, chakula na vipodozi vilivyoteketezwa na mamlaka yake kwa mwaka 2010/2011 ni Sh844. 3 bilioni.

Madhara
Sonda anasema kuwa matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu kwa kaisi kikubwa husababisha maradhi ya figo, fangasi, saratani ya ngozi, ini na mzio.
Mfamasia katika Hospitali ya Amana, Christopher Masika anasema kuwa Serikali pamoja na wadau wengine wa afya hawana budi kuwafundisha Watanzania namna ya kubaini dawa bandia.

Anasema kwamba matumizi ya dawa bandia yana madhara mengi. “Kwa mfano Flagyl haitibu malaria bali inatibu vimelea vya maradhi ya tumbo, mtu akinywa kwa lengo la kutibu malaria atakuwa hajatibiwa na ugonjwa wake utakuwa palepale na baada ya siku chache malaria inaweza kujirudia,” anasema.

Anasema kuwa ndiyo maana siku hizi dawa za malaria zinakuwa sugu na watu wanaendelea kuugua ugonjwa huo kutokana na ujanja mbaya unaofanyika.Kuhusu vipodozi vyenye viambata sumu, Famasia Masika alisema kuwa vipodozi vyenye madini ya Zebaki au Mercury husababisha maradhi ya saratani.

“Kwa mfano hydroquinoline, hiki ni kiambata sumu ambacho kinaharibu ngozi, ni rahisi kupata maambukizi ya ngozi kwa sababu ngozi ya mtumiaji inakuwa nyepesi mno.

Mtu huyo si rahisi kupona hata akijeruhiwa,” anasema
Anasema ngozi ya binadamu ina kinga iitwayo ‘therapine’ ambayo hupukutishwa mtu anapotumia vipodozi vyenye viambata sumu.
Hivyo ni rahisi kupata saratani kwa kuwa kinga hiyo huondolewa.

“Lakini pia matundu ya kutolea uchafu yanazibwa, hivyo mwili hautoi uchafu na sumu inabaki mwilini,” anasema Mfamasia Masika
Anasema kuwa mwanamke anayetumia vipodozi hivyo, ngozi yake huwa laini mno na chochote kitakachoingia huiathiri.

Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza anasema kuwa mamlaka hiyo imepiga marufuku vipodozi vyote vyenye viambata sumu, ingawa bado watu wanavitumia.“Madhara yake ni makubwa, mwanamke mjamzito ni rahisi kuzaa mtoto taahira, au mimba ikatoka,” anasema Simwanza.

Daktari wa Magonjwa ya Ngozi wa Kituo cha Afya Centre, Isaack Maro, anasema wanawake wanaotumia vipodozi vyenye viambata sumu huathirika kwa kiasi kikubwa bila kujijua.Anasema madini ya zebaki yanayotumika katika vipodozi vingi hayatoki kwa urahisi mwilini.

Dk Maro anasema madini hayo hujazana mwilini kwa muda mrefu na kusababisha maradhi.
“Watu wanaotumia vipodozi hivyo figo zao huwa zimetoboka kutokana na kuharibiwa na madini ya zebaki” anasema
Pamoja na madhara hayo, wanawake wanaotumia mikorogo ni asilimia 30 Afrika Mashariki.







Ugonjwa wa Sukari

Watu walio na ugonjwa wa Sukari (kama watu wale wengine) lazima watilie mkazo afya yao ya kila siku.Tofauti imo: walio na ugonjwa wa Sukari, kila siku lazima wapime sukari, wafanye mazoezi na wazingatie afya yao. Ikiwa wewe au mtu unayemjua ana ugonjwa wa Sukari na ameamua kuishi maisha yenye afya, basi Sehemu ya Kujifundisha itakuongezea maarifa kuhusu huu ugonjwa na kukuelekeza kuishi ukiwa na afya.

Hatua ya 1: Jifunze kuhusu ugonjwa wa Sukari
Ni vizuri kujua mambo mengi kuhusu ugonjwa wa Sukari ili uweze kuukimu. Hapa ni yale unayotakikana kujua na kufanya.





Uja Uzito Na Ugonjwa Wa Sukari
Vidokezi kwa kina mama waja wazito
Unapojiandaa kusheherekea furaha tele kwa kupata mtoto, ni muhimu ujue namna ya kukabiliana na ugojwa wa sukari. Hapa vidokezi vitano vya kuweka akilini kila mara:
1. Husiana kwa karibu na kundi la maafisa wa afya bora ambao ni pamoja
  • Daktari au muhudumu wa kiafya aliye na ujuzi wa kutunza wagonjwa wa Sukari
  • Daktari aliye na maarifa ya uzalishaji anayeweza kushughuikia matatizo katika uja uzito na ambaye amewahi kushughulikia kina mama waja wazito walio na ugonjwa wa Sukari
  • Daktari wa watoto au wa watoto wachanga ambao wamezaliwa ambaye anajua kutibu shida maalum zinazoweza kuwakumba watoto wanaozaliwa na kina mama wanaougua ugonjwa wa Sukari
  • Muhudumu wa ulaji aliyesajiliwa anayeweza kukupangia na kukubadilishia chakula wakati wa uja uzito na baada ya kujifungu
  • Daktari wa ugonjwa wa sukari anayeweza kukusaidia kukabiliana na ugonjwa huu wakati wa uja uzito.
2. Uwe maakini sana na madawa yako: Iwapo unatumia tembe za ugonjwa wa Sukari, inaweza kuwa vigumu kuendelea nazo wakati wa uja uzito. Daktari wako anaweza kukupa ushauri wa kujitibu kwa kujidunga dawa ya Insulin ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini badala ya kuendelea na hizo tembe.

3. Kagua kiwango cha sukari katika damu yako: vile tu unavyoagizwa na daktari au muhudumu wako wa afya bora.

4. Zingatia ushauri wa mjuzi wa lishe bora: fuata mwongozo wake wa aina za vyakula unavyostahili kuvitumia ili kiwango cha sukari mwilini mwako kithibitiwe.

5. Mazoezi ni muhimu katika kutibu ugonjwa wa Sukari: Haijalishi iwapo wewe ni mja mzito au la. Zungumza na daktari wako akueleze iwapo kuna tatizo lolote linaloweza kutokea iwapo utafanya mazoezi ukiwa mja mzito. Ni muhimu kujua hasa kwa wale ambao wana ugonjwa wa Moyo pamoja na, au kiwango cha juu cha sukari mwilini.

Niko hatarini kiasi cha kwamba naweza kupata ugonjwa wa Sukari?

Wanasayansi wamejitahidihi hasa kutambua kinachosababisha ugonjwa wa Sukari mwilini. Hakuna hatari zilizo wazi za kuonekana kwa macho kwa aina ya kwanza (Diabetes 1). Lakini aina ya pili (Diabetes 2) ina dalili:
Unene – Hii ni dalili ya kwanza hatari.Mtu akiwa mzito, ana nafasi kubwa ya mwili mwake kukataa aina ya dawa ya insulin kwa sababu mafuta huzuia namna mwili hutumia dawa yainsulin.

Ulegevu na uzembe – Maisha ya mtu kukaa tu ndee si mazuri hasa iwapo mtu huyo ni mnene sana. Mazoezi hufanya moyo kupiga vizuri na kuzuia hali mbaya za kiafya mwilini. Mwili ambao una misuli tu ni rahisi kutumia vizuri Insulini kuliko ule ambao umejaa mafuta katika seli (cells). Hivyo basi, mtu anaweza kurahisisha utendaji kazi wa Insulini kwa kusonga hapa na pale. Pia mazoezi hurudisha chini kiwango cha sukari mwilini na hivyo basi kufanya Insulini kufanya kazi yake vizuri zaidi mwilini. Vile vile kupunguza uzito kitu kizuri. Hivyo basi wacha uzembe!

Mazoea mabaya ya kula: Wagonjwa wengi ambao wamepatikana kuwa na aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari pia ni wanene mno. Hawana mazoea mazuri ya ulaji. Chakula kikiwa na mafuta mengi na chakula kilichowekwa kemikali, kile hakina nyuzinyuzi za kutosha, chakula kilicho na kabohaidreti (wanga) nyepesi, vyote huchangia katika kumfanya mtu kupatikana na ugonjwa wa Sukari mwilini. Kula unavyostahiki kwa weza kuzuia aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari au hata kuupindua.

Historia ya familia: Wakati mwingine huwa katika jeni (genes) na unarithishwa katika familia. Watu ambao wana jamaa waliopatikana kuwa na aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari wao wana nafasi kubwa sana kupata ugonjwa huu. Hali ya maisha ya mtu ndio hasa hufanya mtu apate au asipate ugonjwa wa Sukari.




Kifua Kikuu - TB
TB au Kifua Kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na viini viitavyo ‘tubercle bacilli’.
Wengi wetu tuna viini vya TB mapafuni mwetu lakini hii sikumaanisha kwamba tutauguza huu ugonjwa. TB hushika wale ambao wana ukosefu wa kinga mwilini unao sababishwa na kutokula chakula kizuri, matumizi ya madawa ya kulevya au wanaouguza magonjwa mengine.

TB ya mapafu ndio imeenea zaidi. Hata hivyo, viini vya TB vinaweza kusafirishwa kutoka mapafuni kupitia kwa damu hadi sehemu zingine za mwili na kusababisha hivyo viungo viathiriwe na TB.

Viini vya TB hupatikana kwa mate ya muuguzi. Wakati mgonjwa anakohoa, kupiga chafya au kutema mate kiholela, viini vya TB husambazwa kwa hewa. Mwenye afya akiipumuwa hewa hiyo anaambukizwa na mapafu yake inaanza kuwa na vijidonda.

Dalili za TB
• Kikihozi kisichoisha
• Uchovu na kuishiwa kwa nguvu mwilini
• Kupoteza uzito
• Kupoteza hamu ya kula
• Kutokwa na jasho hata wakati kuna baridi
• Maumivu ndani ya kifua
• Kuishiwa na pumzi
• Mate yaliyo na damu au kukohoa damu
Tiba ya TB
Kuna tembe tofauti zinazotumiwa kutibu TB. Dawa hizi hutumika kwa kipindi cha miezi sita au hata zaidi.

Dalili za TB zikingunduliwa mapema, sio lazima mgonjwa alazwe hospitalini.

Hata hivyo,ikiwa ugonjwa umezidi sana, mgonjwa wa TB atakuwa mdhaifu sana na itabidi alazwe hospitalini.

Chini ya Kanuni mpya za utibabu wa TB ulimwenguni, inapendekezwa, wagonjwa wa TB ya kawaida wanapaswa kulazwa hospitalini kwa miezi miwili pekee halafu miezi minne iliyobaki watibiwe wakiwa na jamii zao.


MDRTB ni neno linalotumika wakati viini vya TB vinashinda nguvu dawa moja au mbili zinazotumiwa kutibu TB. Shida kama hii hutokea ikiwa mgonjwa ametumia madawa kwa njia isiotakikana au alianza matibabu akakosa kumalizia ile miezi sita inayohitajika. Kawaida, inachukua miezi sita au zaidi kutibu TB kabisa. Hata hivyo, mgonjwa akianza matibabu, baada ya muda kidogo hujihisi yuko sawa. Ijapo atakatiza matibabu, kuna hatari kwamba viini vilivyo mwilini mwake hujiunda kipya na kujiongezea nguvu hivi kwamba madawa aliyokuwa akitumia hapo mbeleni hayawezi kumtibu tena. TB ya aina ya MDR wakati mwingi haitibiki na mtu ambaye anaugua aina hii ya MDR anaweza kuisambaza vile vile kama TB ya kawaida.


Matibabu ya mgonjwa aliye na MDRTB inagharimu mara ishirini zaidi ya yule aliye na TB ya kawaida. Matibabu ya mgonjwa wa MDRTB yanaweza kuchukua muda wa miezi kumi na nane.


TB ni mojawapo ya magonjwa ambayo huathiri watu walio na virusi vya Ukimwi. Kama una Ukimwi, jihadhari sana usishikwe na TB. Iwapo unajishuku una TB, hakikisha umepimwa na kutibiwa vilivyo
.



Shinikizo la Damu Mwilini – Ukweli wa Mambo
Shinikizo la juu la damu mwilini ni nini?

Namna ambavyo damu yako hupiga kwenye ukuta wa mishipa ya mwili wako huitwa shinikizo. Kwa kawaida shinikizo la damu la mtu hupanda na kushuka siku nzima. Kwa wengine hubakia juu kila wakati. Hawa ndio watu walio na shinikizo la juu la damu mwilini au Hypertension.

Hali hii huweza kuathiri na kuharibu moyo wako, macho na figo. Huzidisha nafasi yako ya kushikwa na ugonjwa wa pigo (Stroke) au hata kushikwa na ugonjwa wa moyo.

Hivyo basi dalili zake ni nini?
Ugonjwa huu hujulikana kama “muuaji mnyamavu” kwa maana, mtu hukaa nao kwa miaka bila kujua. Njia ya pekee ya kujua iwapo una ugonjwa huu, ni kwenda kupimwa shinikizo lako la damu.

Nitazuiaje ugonjwa huu au hata kuutibu?

Jambo la kushangaza ni kuwa, hatua za kuchukua katika kuzuia shinikizo la juu la damu mwilini ni sawa na za kuutibu ugonjwa huu. Jambo muhimu sana ni kuhakikisha kuwa, unapimwa shinikizo lako angalau mara moja kwa mwaka na mhudumu wa kiafya aliyehitimu. Ni muhimu kwa sababu, kipigo cha damu cha mtu kwa kawaida huendelea kupanda maishani mwake. Njia nyingine ni pamoja na; 
  • Kufanya mazoezi ya mwili ya mara kwa mara
  • Uepukane kabisa na kuvuta sigara na kulewa
  • Ule lishe bora lisilo na chumvi
  • Punguza uzani iwapo wewe ni mkubwa

No comments:

Post a Comment