Biashara ya Mtandao ni njia ya kisasa ya usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani hadi kumfikia mteja au mtumiaji moja kwa moja. Hivyo, kiwanda kinazalisha bidhaa tu. Halafu kuna mtu mmoja tu ambaye ni msambazaji anayehusika na kufikisha bidhaa kwa mteja. Katika mfumo wa biashara za kawaida, kiwanda huzalisha bidhaa kasha huwauzia labda Depot au mawakala wakuu. Hawa huwauzia tena wasambazaji au wauzaji wa jumla, nao pia huwauzia wauzaji wa rejareja ambao watamfikishia mteja. Kwahiyo, bidhaa inaweza kuzalishwa kiwandani kwa tsh 380 lakini mteja ataipata kwa tsh 600. Kuna tsh 220 inagawanywakwa watu wa katikati. Lakini hapo hapo utagundua kiwanda hakipati faida kubwa sana kwa sababu, katika hiyo hiyo 380 kuna gharama za usambazaji, kuwalipa macelebrities kwa ajili ya matangazo, radio, television, mabango, magazeti na hata mitandao ya kijamii, pamoja na gharama za sales department na mengineyo. Mwisho wa siku, utakuta kiwanda unaweza kukuta katika 380, baada ya kutoa gharama zote labda 180 ndiyo inaweza kubaki kama faida.

Katika biashara ya mtandao, ile 220 ambayo inagawanywa kwa watu wa katikati, anapewa mtu mmoja tu ambaye ni msambazaji atakayenunua bidhaa toka kiwandani kwa tsh 380 na kumfikishia mtumiaji kwa tsh 600. Hivyo, kiwanda hakitalipia tena gharama za matangazo, mabango pamoja na nyingine ila kitamuelimisha huyo msambazaji kuhusu bidhaa ili yeye sasa aweze kumfikishia mtumiaji moja kwa moja. Hivyo kiwanda kinampa msambazaji uhuru wa kuwashirikisha watu wengine ambao watakuwa washirika wake katika biashara ili aweze kukuza biashara yake. Atawafundisha hao washirika wake katika biashara ili nao wawe na uwezo wa kufanya kama yeye. Lakini atanufaika kwa kila mtu anayemshirikisha katika biashara kwa kupata asilimia za mauzo ya hao pamoja na timu zao

Atakuwa amegawa muda wake vizuri na kutengeneza kipato kizuri hata yeye asipofanya kazi, endapo atajenga timu. Lakini tambua kila mmoja ana fursa sawa ya kutengeneza kipato. Kipato kikubwa hutegemea jinsi mtu atakavyokuwa na timu kubwa kwa kuwashirikisha watu wengi katika biashara. Msingi wa hii biashara ni kushirikishana habari kuhusu bidhaa au huduma inayotolewa na kampuni halafu unanufaika na kutengeneza kipato. Lakini una uhuru wa kuanzisha kampuni yako `invisible company` ambapo utafanya biashara na kampuni na kutanua wigo wa biashara yako kwa kuwekeza muda wako kuwafundisha wengine biashara ambao watakuwa washirika wako kwenye biashara kwa kuwa na kipato kisichokuwa na kikomo.

Hayo ni maelezo mafupi tu kuhusu biashara ya mtandao japo ni biashara kubwa sana na inahitaji kujifunza kwa kina na kuielewa kwani ili ufanikiwe katika biashara ya mtandao lazima ujifunze upate kuielewa vizuri, hapo utafanikiwa. Nimekutana na watu wengi walioshindwa hii biashara, karibia wote nimegundua hawakuwa na uelewa mzuri wa biashara. Hapa huhitaji pesa ili utengeneze pesa, ila unahitaji maarifa. Kama huna maarifa ya kutafuta pesa unaweza leo ukashinda tuzo ya shilingi million 100, lakini baada ya miez 3 ukawa kapuku wa kutupwa!.

Kuna watu wengi maarufu duniani wanaoamini katika hii biashara akiwemo Robert Kiyosaki Mwandishi wa vitabu vya Rich dad poor dad pamoja na vingine kama The business of 21st century. Ameelezea vizuri sana hii biashara. Lakini yupo Professor Pat Utomi wa Pan African University anasema `Network marketing is the futuristic way of doing business now`. Bwana Bill Clinton pia katika hotuba yake alikuwa akiyashukuru makampuni ya network marketing kwa kuwapa watu fursa sawa na kubadilisha maisha yao. Lakini pia Bill Gates, aliwahi kuulizwa kama angefilisiwa na kuanza upya angefanyeje?. Yeye alisema tu kwamba angechagua biashara ya mtandao. Lakini wapo wengine wengi wanaoiamini na kuwashauri watu wanaotaka mabadilko waifanye.

Kuna makampuni zaidi ya 5,000 yanayofanya biashara ya mtandao duniani. Hivyo unapotaka kufanya jaribu kuangalia kampuni bora. Mimi kampuni ninayofanya nayo, iko katika kumi bora kidunia kwa miaka mingi sana. Kwa Afrika na Tanzania ni namba moja. Nakushauri pia wewe unayependa hii biashara, usikurupuke ilimradi biashara ya mtandao, ila angalia kampuni itayokufaa. Lakini biashara ya mtandao sio `get rich quick scheme`, japo kuna watu wanatengeneza pesa nyingi ndani ya muda mfupi sana na kubadilisha maisha yao. Ni kitu ambacho kwa wakati mwingine kitakuchukua muda kuyapata mafanikio. Inaweza kukuchukua pengine hata mwaka mmoja kuanza kuona matokeo makubwa/kutoboa kama waswahili wanavyosema. Ila mafanikio yakija/ ukitoboa tambua huwa ni ya kudumu.

Unapoamua kufanya biashara hii usimsikilize mtu, ielewe biashara halafu uamue kama inakufaa kwa kulinganisha marketing plan na ndoto zako. Ukiona inakufaa, nakushauri anza maramoja. Ukitaka ushauri kutoka kwa watu utakutana na watu wa aina 3. Aina ya 1 ni wale wasiojua lolote kuhusu hii biashara na watakwambia haifai. Kundi la 2 ni wale waliowahi kuisikia, huenda hata kuifanya halafu wakashindwa. Hao watakupa sababu za kushindwa. Aina ya mwisho ni wale wanaofanya na wamefanikiwa na wanakushauri uifanye na kukuahidi sapoti ya kutosha. Nakuomba usikilize hili kundi la mwisho. Tambua hili ni kundi dogo sana kwani dunia imegawanyika, wengi ni watu wenye mtazamo hasi, waoga na hawana ndoto kubwa, au wana ndoto kubwa ila huacha hofu kuwazuia kufanya maamuzi sahihi.

Mi nakumbuka nilipoambiwa mara ya kwanza kuhusu hii biashara, kuna rafiki zangu wa karibu sana walinivunja moyo na kunikatisha tamaa. Mimi sikuwasikiliza kwa sababu nilijua maisha ni yangu na nimeshaona fursa. Nilianza kuifanya kwani niliona waliofanikiwa kupitia biashara hii. Hii ni biashara ambayo imerudisha ndoto zangu zilizokuwa zimepotea kwani naona namna nitakavyoweza kutimiza ndoto zangu kupitia hii biashara. Hii biashara inaweza kumtimizia mtu yeyote ndoto zake endapo atakuwa na fikra sahihi na kujifunza biashara. Ila sisi tuko tayari kutoa sapoti kwa yeyote anayetaka kuanza hii biashara ili kuhakikisha anafanikiwa nasi tuweze kufanikiwa pia kwani huu ndio msingi wa biashara hii. Kama una roho mbaya huwezi kufanikiwa hata kidogo na hii biashara haikufai, nakushauri tafuta biashara nyingine. Hii ni biashara ya watu wanaopenda kuwasaidia wengine pia wafanikiwe.

Hizi ni baadhi ya sababu, kwanini ufanye biashara ya soko la mtandao: 1. Mtaji kidogo. Hii biashara haihitaji mtaji mkubwa sana. Mtaji unaoweza kuanza nao ni 750,000/ kima cha juu, lakini pia mtu waweza kuanza na mtaji wa sh 375,000/. Lakini haihitaji duka, wala haihitaji kutembeza bidhaa mtaani kama machinga wala haihitaji vibali. Kampuni imeandaa mfumo mzuri wa kuuza bidhaa ambao tunautumia. Lakini unapofanya nasi unapata free license ya kufanya biashara ktk nchi zaidi ya 160 duniani.

2. Mafunzo ya biashara bure na usaidizi. Kampuni imeandaa mfumo mzuri wa biashara ambapo utapata mafunzo ya biashara na usaidizi wa karibu hadi uwe na uwezo wa kusimama na kuitanua biashara yako kitaifa au hata kimataifa.

3. Flexibility. Hapa nazungumzia uhuru wa kupanga muda wako katika kuifanya biashara yako. Unaweza kuifanya kwa muda wako wa ziada angalau  lisaa kwa siku, au masaa 10 kwa wiki au unaweza kuamua kuifanya kwa muda wako wote. Watu wengi huanza kwa muda wa ziada, wakiona wamefanikiwa hufanya kwa muda wote.

4. Vipato vikubwa. Ni biashara ambayo itakupa vipato vikubwa ndani ya muda mfupi sana ukilinganisha na biashara zingine nyingi. Jitihada zinahitajika ili kuijenga biashara yako iweze kukua na kukupa faida kubwa. Kitu cha msingi ni kuwa na uelewa mkubwa wa hii biashara. Lakini ukifanya nasi biashara katika kampuni yetu utakutana na njia zaidi ya 10 za kutengeneza vipato katika kampuni. Ndiyo maana watu wanatengeneza vipato vikubwa sana.

5. Uwezo wa kuikuza biashara yako mahali popote pale duniani. Hii ni fursa ambayo unaipata katika hii biashara bure kwa kufanya biashara na watu sehemu nyingine duniani bila ugumu hata pengine wewe usipokuwepo huko. 6. Inarithika. Kitu ambacho nakipenda sana katika hii biashara ni kuweza kuirithisha. Utakapoishia ndipo yule mrithi wako ataanzia na kuendeleza. Hivo unapofanya hii biashara tambua umefanya investment ya maisha yako na vizazi vyako.

7. Ina rasilimali muda `leverage` hii ni siri kubwa sana ya mafanikio katika biashara yeyote kubwa na ndio msingi wa mafanikio. Watu wote waliofanikiwa katika biashara zao kubwa ni wazi kuwa wamewekeza katika rasilimari muda.

8. Ni njia pekee ya kumiliki biashara kubwa duniani. Hii biashara ina sifa zote za biashara kubwa, biashara yeyote kubwa ina mambo makuu 3 yafuatayo; Bidhaa/huduma, mfumo pamoja na Timu au watu wanaofanya kazi. Kwa Tanzania ili biashara iitwe kubwa lazime uwe na watu kuanzia 100 wanaokufanyia kazi. Kidunia idadi inayotakiwa ili iitwe biashara kubwa ni kuanzia watu 500. Lakini hii biashara unaweza kuwa idadi kubwa zaidi ambapo utakuwa na watu ambao hujawaajiri wala huwalipi mshahara ila umewekeza muda wako kuwafundsha biashara ili wafanye kile unachofanya waweze kufanikiwa nawe ufanikiwe maradufu.

9. Ni biashara ya kisasa ambayo inakwenda na wakati. Kila fursa ina wakati wake. Huu ndio wakati muafaka wa hii fursa. Hapa kwetu Tanzania imeanza muda sio mrefu sana lakini imebadilisha maisha ya watu wengi.

10. Imejengwa katika dhana ya DUPLICATION ambayo kwa mujibu wa Mwanasayansi Robert Einstein aliandika katika moja ya vitabu vyake kuwa; mfumo wowote unaobeba dhana hii itakuwa ni maajabu ya 8 ya dunia. Ziko faida nyingi sana na kuna picha kubwa sana ya biashara ambayo unatakiwa kuielewa kama wewe ni mtu makini, una ndoto kubwa na unahitaji mabadiliko ya kweli katika maisha yako.

Jukumu letu ni kukusaidia na kukuongoza ili kuhakikisha unafanikiwa. Kama umevutiwa na unapenda kujua zaidi kuhusu biashara hii. Tuwasiliane, ili nikuoneshe marketing plan yetu, ukipenda tuanze biashara. Ila nahitaji watu ambao wako serious tu, wenye ndoto kubwa na mtazamo sahihi, ambao wako tayari kujifunza kupitia wengine ambao wanafanya hii biashara na wamefanikiwa.

Hii biashara sio ya kila mtu, hivyo ndivyo mimi naamini na ndivyo ilivyo. Hii ni biashara ya watu ambao wanahitaji mabadiliko katika maisha yao. Mabadiliko huanza na kubadili fikra. Tuna msemo kuwa, huwezi kubadili maisha yako ikiwa hauko tayari kubadili fikra zako. Huwezi kufika sehemu tofauti endapo fikra ni zilezile na matendo ni yaleyale. Watu waliofanikiwa wanafikiria tofauti, eti?. Asante kwa kusoma.