PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Monday, September 30, 2013

Furahia Maisha: 25 Common Characteristics of Successful Entreprene...

Furahia Maisha: 25 Common Characteristics of Successful Entreprene...: Do you have what it takes to get through hard times? Here are the traits that help home-based business owners thrive. 1. Do what you enjoy...

25 Common Characteristics of Successful Entrepreneurs.:

Do you have what it takes to get through hard times? Here are the traits that help home-based business owners thrive.

1. Do what you enjoy.
2. Take what you do seriously.
3. Plan everything.
4. Manage money wisely.
5. Ask for the sale.
6. Remember it's all about the customer.
7. Become a shameless self-promoter (without becoming obnoxious).
8. Project a positive business image.
9. Get to know your customers.
10. Level the playing field with technology.
11. Build a top-notch business team.
12. Become known as an expert.
13. Create a competitive advantage.
14. Invest in yourself.
15. Be accessible.
16. Build a rock-solid reputation.
17. Sell benefits.
18. Get involved.
19. Grab attention.
20. Master the art of negotiations.
21. Design Your workspace for success.
22. Get and stay organized.
23. Take time off.
24. Limit the number of hats you wear.
25. Follow-up constantly.

TATIZO LA UKOSEFU/ UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

 Chanzo,Athari & Suluhisho Lake.
Wanaume wengi wanasumbuliwa na tatizo
la ukosefu/ upungufu wa nguvu za kiume,
hii ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za
kitaalamu. Hapa kwetu hususani katika
maeneo ya mijini, katika kila wanaume
kumi wanao tembelea barabarani angalau
watatu kati yao wanakabiliwa na tatizo la
upungufu/ ukosefu wa nguvu za kiume,
wamewahi kukabiliwa na tatizo hilo ama
hawana uhakika kama wanazo nguvu za
kiume za kutosha.

 Tunazo shuhuda nyingi
sana za watu wanao sumbuliwa na tatizo
la nguvu za kiume ambao wanakuja
kupata tiba na ushauri kituoni kwetu
lakini kwa sababu za ki-ethics hatutoweza
kuzipublish hapa mtandaoni, ila kiukweli
tatizo la upungufu ama ukosefu wa nguvu
za kiume lisipo tafutiwa ufumbuzi wa kina,
linaweza kuwa na athari kubwa sana kwa
muhusika katika maisha yake yote.
 

Ukosefu wa nguvu za kiume ni nini?
Ni hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo
wa kufanya/ kukamilisha tendo la ndoa
kwa ufasaha..
Mwanaume mwenye nguvu za kiume ni
yupi?
Mwanaume mwenye nguvu za kiume ni
yule mwenye uwezo wa kufanya/
kukamilisha tendo la ndoa kwa ufasaha.
 

CHANZO CHA UKOSEFU WA NGUVU ZA
KIUME
Kwa ufupi sana, hizi ni baadhi ya sababu
zinazo sababisha upungufu wa nguvu za
kiume kwa wanaume.
1. Msongo wa mawazo
2. Ulevi kupita kiasi.
3.Kupooza kwa mwili
4. Presha na ugonjwa wa kisukari.
5.Wasiwasi wa kutekeleza tendo la ndoa
6. Uoga wa kufanya tendo la ndoa.
7.Uzoefu wa kukatisha tamaa wa siku za
nyumaa
8.Chango la kiume.
9. Kuugua ugonjwa wa ngiri
10. Mazingira yasiyoridhisha wakati wa
tendo la ndoa.
11. Ulaji mbovu wa vyakula haswa haswa
ulaji wa vyakula vya mafuta kwa wingi
kupita kiasi.
12. Kufanya masturbation kwa muda
mrefu n.k
 

ATHARI ZA UPUNGUFU / UKOSEFU WA
NGUVU ZA KIUME
Ukosefu ama upungu wa nguvu za kiume
una athari nyingi sana, zifuatazo ni baadhi
ya athari za ukosefu/ upungufu wa nguvu
za kiume.
1. Kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi.
2. Kuvunjika kwa ndoa.
3. Kujiua : Baadhi ya wanaume hufikia
uamuzi wa kujiua baada ya tatizo kuwa
kubwa na kutumia dawa za aina
mbalimbali bila mafanikio.
4. Upungufu wa nguvu za kiume
huongeza chachu ya maambukizi ya v.v.u
kwa wanandoa.Tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume linapokuwa sugu,
hupelekea rafiki wa kike/ mke wa
mwanaume anaye sumbuliwa na tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume, kutoka nje
ya ndoa kwa ajili ya kutimiziwa haja zake
za kimwili, mwisho wa siku mwanamke
huyo huweza kumletea magonjwa mume
wake mwenye tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume pindi wanapokutana
kimwili katika hali hiyo hiyo ya
kutoridhishana
5. Ulevi kupita kiasi ; Wakati mwingine
wanaume wanao sumbuliwa na tatizo hili,
huamua kuwa walevi kupita kiasi ili
angalau kupunguza mawazo.
Kwa ufupi ukosefu/ upungufu wa nguvu za
kiume ni tatizo kubwa sana ambalo
endapo halitatafutiwa usumbufu na
muhusika linaweza kuyaathiri maisha ya
muhusika kwa kiasi kikubwa sana.

UMUHIMU WA NDIZI MBIVU KATIKA AFYA YAKO

Baada ya kusoma makala yangu ya leo na kuzingatia nilichokiandika, bila shaka utaanza kuiangalia ndizi kwa mtazamo tofauti na uliokuwa nao hapo awali. Ndizi mbivu ni tunda maarufu sana duniani lakini ni watu wachache wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo kwenye tunda hili.

Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose na Glucose na vilevile ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre) ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.

Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya muda wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda muhimu sana kwa wanamichezo. Hata hivyo, nishati siyo faida pekee unayoweza kuipata katika ndizi, ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na kuzuia matatizo mengi ya kiafya:

MFAIDHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.

MATATIZO WAKATI WA HEDHI (PMS)

Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.


UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)

Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upunguvu wa damu kwa sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.

SHINIKIZO LA DAMU

Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.

Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.

NGUVU YA AKILI

Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti unaonesha kuwa potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kujisomea.

KASUMBA (HANGOVERS)

Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover) ni kunywa ‘Milkshake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.

Mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo juu, ndizi pia husaidia katika matatizo mengine mengi kama vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa asidi tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.k

Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora, ukiilinganisha na Tufaa (Epo (Apple), ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili, vitamin A na chuma mara tano na vitamini na madini mengine mara mbili zaidi ya tufaa. Mwisho; USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU!

ZIJUE ATHARI ZA KUPIGA PUNYETO

Wanaume waliowengi hukidhi haja zao kwa kutuliza matamanio yao kwa njia ya kujichua/ kupiga punyeto bila kufahamu madhara yake: Nikweli punyeto inasaidia kupunguza hamu ya tendo na ni njia nzuri ya kujiepusha na zinaa kwa kujilinda na maradhi ila kiukweli ina madhara na madhara yake mara nyingi hutokea kwa mtu anaependelea sana kupiga punyeto, kutokana na utafiti uliofanywa kisayansi imeonekana punyeto ni nzuri kiafya ila endapo kama utakuwa unapiga mara moja moja na sio kila siku. Napenda kuwashauri watu wanaopiga punyeto wawe makini na wasiendekeze jambo hili kwani madhara yake ni makubwa sana na Athari zake kubwa ni hizi zifuatazo:

1. PUNYETO INAUA NGUVU ZA KIUME
2. KUWAHI KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO
3. Kupunguza uwezo wa kufikiri.
4. Kukosa nguvu katika magoti.
5. Madhara ya ndani ya sehemu za siri.
6. Kutofurahia tendo la ndoa.

MADHARA SABA KWA WANAUME WAOPENDA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

Leo tunageuza shilingi upande wa pili kuelezea madhara ya kuruka ukuta (kufanya ngono kinyume cha maumbile), baada ya kuona madhara ya wanawake kurukwa na nini kifanyike.

Wanaume wengi walinilaumu na kuniona sitendi haki kwa kuwaelezea wanawake tu wakati mchezo huwa una athari kwa mtenda na mtendewa.

Kama nilivyoelezea kwenye mada za wiki kadhaa zilizopita, mchezo huu unatumika sana katika mapenzi ya sasa, watoto wa mjini wana usemi wao kwa kitu kilichovuma kuwa ‘ndiyo habari ya mjini’.

Mchezo huu umekuwa ukipendwa sana na wanaume wengi ambao wengi wao huwa hawatumii kinga na kusababisha wengi kupata magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Lakini mchezo wa kuruka ukuta umekuwa na madhara makubwa sana kwa wanaume wanaoufanya kwa muda mrefu.

Tulipoangalia upande wa wanawake, tuliona sehemu kubwa ya wanaopenda mchezo huu ni wanaume ambao wengine wamebatizwa majina ya ‘basha’, wakimaanisha mwanaume mpenda kuruka ukuta bila kuangalia ni wa mwanaume mwenzake au wa mwanamke.

Kwa vile nia ya kona hii ni kuelimisha madhara ya mtu kupenda kuruka ukuta ili aache mara moja, tunaendelea kutoa elimu ya bure ili mtu yakimkuta ajue yamempata kwa kiburi chake na kwa kupenda starehe ya kipuuzi.

Madhara anayoyapata mwanaume anayependa mchezo huo ni kama ifuatavyo:

Kwanza: Husababisha kusinyaa au kuweka makovu kwenye njia ya haja ndogo.

Pili: Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba kabisa.

Tatu: Kupata saratani (kansa) ya tezi za figo (prostate gland).

Nne: Kupata magonjwa sugu ya uti wa mgongo.

Tano: Kuharisha.

Sita: Maambukizi ya VVU ambapo mwisho wake ni Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi).

Saba: Baadaye mhusika kupata msongo wa mawazo au sonona kwa kujutia tendo hilo.

Nina imani ndugu yangu umeona madhara mabaya sana ya tabia hiyo mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia wenzako na kuona raha lakini tumeona madhara yake, ambayo kwa hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa kuacha mara moja kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.

Jiepushe kuiga mambo bila kujua faida na hasara zake pia usimtie mwenzako majaribuni kwa kumlazimisha kuingia kwenye mchezo huo. Wanawake wengi wamekuwa wakilazimishwa na wanaume kuingiliwa kinyume na maumbile kwa kuwatishia kuwaacha kama watakataa.
Swali linakuja, kipi bora, kuharibiwa au kuachana?
Kumbuka baada ya kuharibikiwa, thamani yako hushuka na sifa yako ikiwafikia waharibifu wa watu, basi unageuzwa jamvi la mtaa na hatimaye unakufa kwa msongo wa mawazo au mateso ya ugonjwa utakaupata baada ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.

Unaweza kushangaa baada ya kuelezea madhara yanayowapata wanaume nimehamia kwa wanawake. Ukweli mchezo huu umewaathiri sana wanawake ambao wengi wanaujutia.

JE, UNAUFAHAMU UGONJWA WA KISUKARI?

Kisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini.

Aina za Kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo;
1. Aina ya kwanza ya Kisukari au Type 1 Diabetes Mellitus
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana (young adults).
Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans katika tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

2. Aina ya pili ya Kisukari au type 2 Diabetes Mellitus
Hii ni aina ya kisukari inayotokea zaidi ukubwani. Aina hii ya kisukari husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.
Hali hii husababishwa na unene uliopitiliza yaani obesity, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa (physical inactivity).
Kwa vile, katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi wa utendaji kazi wake, wagonjwa wa aina hii ya kisukari hawahitaji kupewa insulin kwa njia ya sindano. Ndiyo maana aina hii hujulikana pia kama kisukari kisichotegemea insulin au Non Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM)

3. Kisukari cha Ujauzito (Gestational DM)
Ni aina ya kisukari kinachotokea pindi kunapokuwa na ongezeko la kiwango cha sukari katika damu (hyperglycemia) wakati wa ujauzito. Aina hii ya kisukari huathiri karibu asilimia 2-5 ya mama wajawazito wote ingawa wengi wao hupata nafuu na kupona kabisa mara tu baada ya kujifungua.

Viashiria vya ugonjwa wa kisukari (risk factors)
• Unene uliozidi na kiribatumbo
• Ulaji mbaya wa chakula
• Baadhi ya madawa
• Msongo wa mawazo
• Historia ya ugonjwa wa kisukari kwenye familia
• Tezi ya shingo (husababisha mwili kukua na kuongezeka haraka)
• Kutofanya mazoezi
• Umri zaidi ya miaka arobaini (kadri tunavyozeeka na kongosho letu linapungua uwezo wa kutoa insulin hivyo kusababisha kisukari)
• Magonjwa yanayoharibu kongosho
• Akina mama wanaojifungua watoto wenye kilo zaidi ya arobaini (Mara nyingi hawa akina mama huwa na ugonjwa wa kisukari ila hawagunduliki hadi mtoto anapozaliwa na kuonekana mkubwa)
• Akina mama wenye historia ya kisukari wakati wa ujauzito
• Utumiaji uliozidia pombe na uvutaji sigara

Dalili za ugonjwa wa kisukari
• Kiu ya mara kwa mara
• Kupungua uzito licha ya kula vizuri
• Njaa kali na ya mara kwa mara
• Jasho jingi
• Uchovu usioeleweka hata bila kufanya kazi
• Kizunguzungu
• Macho kupungua uwezo wa kuona
• Kidonda kisichopona haraka

UMUHIMU WA MAZOEZI KWA MWANAMKE MJAMZITO.

 
Leo tutaongelea mazoezi gani ya kawaida ambayo mama mjamzito anaweza kuendelea kuyafanya kila siku ya ujauzito wake na umuhimu wake.

Mazoezi wakati wa ujauzito yanasaidia:
Kupata usingizi mzuri usiku.
Kuondoa stress
Kulegeza na kunyoosha misuli ya uzazi na kuitayarisha kwa kazi ya kujifungua
Kupunguza kichefu chefu(morning sickness) na kiungulia(heartburn)

KUMBUKA:
Wakati unafanya mazoezi hakikisha kuwa husikii maumivi yoyote na ukipatwa na maumivu hakikisha unaonana na daktari haraka iwezekanavyo. Kumbuka usilalie mgongo wakati wa kufanya mazoezi au usifanye mazoezi aina ya jogging(kukimbia) au kuruka ruka(bouncing) na hakikisha mdundo wa moyo(pulse) na temperature yako ya mwili ziko sawa. Kunwya maji mengi kuzuia dehydration na angalia balance yako iko sawa ili kuzuia kuanguka.

Kama ulikuwa unafanya mazoezi kabla ya ujauzito unaweza kuendelea na mazoezi yafuatayo:

.Kuogelea: Uzuri wa zoezi hili ni kwamba halihitaji nguvu nyingi linasaidia kurelax na misuli yote ya mwili inafanya kazi. Unaweza kuogelea kwa dakika 20 hadi 35 lakini uchukue break pale utakapoona umechoka au kuishiwa na nguvu au pumzi. Kuogelea pia kunasaidia kupunguza maumivu yatokanayo na miguu kuvimba.
.Kutembea: Ni zoezi zuri sana kwa mwanamke mjamzito. Zoezi hili linaweza kufanywa dakika 20 had 35 kwa siku. Zoezi hili linapunguza stress, linasaidia chakula kushuka vizuri na digestion. Pia linasaidia katika kuweka sawa uti wa mgongo. Tatizo la uti wa mgongo kutokunyooka linasababishwa na tumbo kuongezeka na kukosekana kwa balance kwenye mwili. Hiki ni chanzo cha maumivu ya mgongo. Kumbuka kuchuka break na kupumzika pale utakaposikia uchovu.
.Kucheza Muziki: Mama mja mzito anaweza kucheza mziki kama zoezi hasa hasa mziki wa belly dancing wa kunyonga kiuno na miziki aina ya salsa. Hii inasaidia katika kulainisha misuli ya uzazi tayari kwa kujifungua, kusaidia kujifungua kwa urahisi na kupona kwa haraka zaidi baada ya kujifungua, kupunguza michirizi ya tumbo(stretch marks) inayojitokeza kwa ajili ya ngozi ya tumbo kuvutwa, pia inasaidia confidence ya mwanamke kujiona bado ana mvuto, kuondoa stress, kusaidia na balance, kupunguza maumivu ya mgongo na kusaidia kunyoosha uti wa mgongo.
.Pia unaweza kuendesha baiskeli ila uangalie balance usianguke na usiendeshe sehemu zenye msongamano wa watu au traffic ikiwezekana tumia baiskeli special za mazoezi ndani ya gym(stationary bikes).

MAJI: TIBA KUBWA KULIKO ZOTE.:

Tuangalie ni kwa kiasi gani maji ni tiba kubwa kuliko zote mwilini. Mwili wa binadamu unategemea maji kwa kiasi kikubwa na unapokosa au kupungikiwa, hutoa ishara zake ambazo wengi wetu hatuzijui. Ishara hizo zinapopuuzwa huzaa matatizo mengine ya kiafya.

Kwa uchache, binadamu anatakiwa kunywa maji yasiyopungua glasi nane kila siku. Kiwango hicho kitaongezeka iwapo mtu ana uzito mkubwa na shughuli zake nyingi zinatumia maji mengi mwilini. Hivyo kiasi hicho cha glasi nane ni kiwango cha chini kabisa anachotakiwa kunywa mtu hata kama hana kazi yoyote.

Ifuatayo ni orodha ya magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa kunywa maji. Vile vile utajua baadhi ya dalili na madhara yanayojitokeza mwili unapoendelea kukosa maji:

1: Maji hutibu kiungulia (heart burn)
Kiungulia ni dalili kwamba mwili una upungufu mkubwa wa maji. Mara nyingi watu wanaposumbuliwa na kiungulia hudhani tumbo limejaa gesi hivyo kukimbilia kumeza vidonge ili kutuliza maumivu, lakini tatizo la upungufu wa maji huendelea kuwepo.

Bila kujua kuwa kiungulia kinatokana na kutokunywa maji, mtu huyo huendelea kumeza vidonge. Matokeo yake hali ya upungufu wa maji inapoendelea kwa muda mrefu, husababisha madhara mengine kama kuvimba tumbo, henia, vidonda vya tumbo na hatimaye kupatwa na saratani ya tumbo, maini na mapafu.

2: Maji hutibu baridi yabisi (Arthritis)
Maumivu ya kwenye mauingio ya mwili (baridi yabisi), hasa magoti, ni dalili nyingine ya upungufu wa maji katika sehemu hizo. Ni ugonjwa unaoweza kumpata mtu mzima na mtoto. Umezaji wa vidonge vya kupunguza maumivu hakuondoi tatizo, bali hufanya hali kuwa mbaya. Kunywa maji mengi na chumvi kidogo kunaweza kuliondoa tatizo kabisa.

3: Maji huzuia na kutibu maumivu ya mgongo
Maumivu ya kiuno na uti wa mgongo nayo ni dalili ya upungufu wa maji katika sehemu hizo, hasa katika maungio ambayo yanabeba uzito wa mwili. Maumivu ya aina hii hutibiwa kwa kuongeza kiwango cha kunywa maji na siyo madawa.

Mtu akiendelea kunywa dawa za kupunguza maumivu bila kuongeza kiwango cha maji mwilini, madhara yake huwa makubwa. Viungo huendelea kuathirika na hatimaye kudhurika kabisa na hivyo kumsababishia mtu ulemavu au upasuaji ambao humuachia maumivu siku zote yatakayomfanya kuwa mtumwa wa dawa.

4: Maji hutibu maumivu ya moyo (Angina)
Maumivu ya moyo nayo huwa ni dalili ya upungufu wa maji katika njia ya moyo na mapafu. Hali hiyo inapotokea, inatakiwa kutibiwa kwa kunywa maji mengi kila siku na siyo kukimbila kunywa dawa za kutuliza maumivu (pain killers).

WAJUA MADHARA YA KUJICHUBUA?

Leo tunaongelea swala la kujichubua.

Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango, hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.

Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.

Madhara ya kujichubua ni yapi?

Mtu aneyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.

NINI KISABABISHACHO MWANAMKE KUKOSA HEDHI (AMENORRHEA)

Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).

Primary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au nywele za kinena; au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.

Secondary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.
Mwanamke hupataje hedhi?

Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus napituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.

Amenorrhea husababishwa na nini?
Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.

1. Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.

1. Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na
-Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary
-Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi. Ugonjwa huu hujulikana kama Kallmann syndrome
-Lishe duni na utapia mlo
-Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza)

2. Matatizo katika tezi ya Pituitary: Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na
- Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamuProlactinemia. Prolactin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.
-Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.
-Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
-Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
-Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

3. Matatizo katika ovary: Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na
-Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)
-Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia)
-Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa
-Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake
-Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao humbatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida. Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease)
-Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji
-Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili
-Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary
-Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu

2. Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi: Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na

1. Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke, shingo ya uzazi au mji wa mimba (uterus)

2. Kuta za uterus zinazotazamana kujishikiza pamoja

3. Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen)

4. Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka

3. Mabadiliko katika mwili wa mwanamke: Mambo yanayoweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na

1. Kula kiasi kidogo sana cha chakula kuliko kawaida au kula kupita kiasi
2. Unene uliopitiliza au kupungua uzito/kukonda isivyo kawaida
3. Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu
4. Utapiamlo
5. Msongo wa mawazo
6. Matumizi ya madawa ya kulevya
7. Matumizi ya baadhi ya madawa hususani baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili
8. Kuwa na hofu iliyopitiliza
9. Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi

Dalili za Amenorrhea ni zipi?
Kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na
• Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo
• Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen
• Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovary
• Kuongezeka uzito kupita kiasi au kupungua kwa uzito isivyo kawaida
• Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida yaweza kuashiria kuwepo kwa matatizo ya kiakili na kisaikolojia

Je kukosa hedhi kunaweza kusababisha nisipate mtoto?
Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo halitashughulikiwa.

Wednesday, September 11, 2013

ZIJUE MBINU ZA KUBADILISHA MAISHA YAKO NA KUFANYA YAWE MAZURI NA YENYE MAFANIKIO.

Wanadamu wote tumeumbwa na kupewa akili ambayo inabidi tuitumie vizuri ili kuweza kuishi vyema katika ulimwengu huu. kinachoshangaza ni kwamba wapo watu wachache tu ambao wamekuwa wakitumia akili vizuri na kufanya vitu vikubwa vinavyo wapatia mafanikio makubwa, huku wengi wetu tukiwa tumebaki kusema kuwa wao wamebahatika.

Hakuna watu waliozaliwa na bahati au mikosi, wanadamu wote wanauwezo wakutumia akili vizuri na kujipatia kipato kikubwa sana. yapo mambo kadha wa kadha ambayo inabidi tuweze kuyafanya ili kuhakikisha kuwa tunasonga mbele na kuwa na maisha mazuri.

kwanza kabisa, lazima mtu uwe na nidhamu katika kila kitu ambacho unakifanya. nidhamu inachukua sehemu kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria. hakikisha unakuwa na ratiba inayoeleweka ambayo itakuwa inakuongoza katika shughuli zako za kila siku. hii itaongeza ufanisi, lakini pia nidhamu humfanya mtu aheshimike na kuoneka ana thamani katika jamii, kitu kinachoweza kufanya watu wakupatie kazi mbalimbali kwakuwa wanaamini hauta waaibisha.

Uwe mwaminifu katika maisha yako. uaminifu umekuwa adimu sana kwa watu wengi, jambo linalopelekea watu kukosa nafasi mbalimbali kwakuhofiwa kufanya ubadhilifu. ukiwa mwaminifu ni rahisi kupata fursa nyingi na kazi nzuri zenye maslahi mazuri. uaminifu ni silaha kubawa sana katika maisha.watu waliofanikiwa walikuwa waaminifu kwa sehemu kubwa, hawakuwa na tamaa ndogondogo zisizo nafaida. hakuna haja ya kuiba fedha kidogo ambazo zitachafua jina lako na kufanya heshima yako ipotee. kumbuka kuwa ni rahisi sana kupoteza heshima kuliko kuijenga.

Usiwe na matumizi yasiyo na msingi. watu wengi hawafanikiwi kwasababu wanatamani maisha ya wenzao, wanapenda waonekane wana maisha ya juu wakati sio kweli. hakuna haja ya kutafuta sifa mbele za watu wakati ukirudi kwako unaanza kujuta kwa matumizi uliyoyafanya. weka akiba kwa kile unachokipata, achana na starehe zisizo za msingi. unywaji wa pombe unafilisi sana na unakwamisha sana maendeleo ya watu wengi. ishi maisha yaliyo ndani ya uwezo wako, ukiwaza kupiga hatua na si kudumaa hapohapo ulipo.

Fanya kazi kwa bidii na kwa malengo ili uwe na maisha mazuri. uvivu wa kufikiri na wa kufanya kazi unakwamisha maendeleo. tazama watu wote waliofanikiwa wanafanya sana kazi kwa bidii. Mwenyezi Mungu alisema kuwa asiyefanya kazi na asile, usichague kazi ya kufanya ilimradi isiwe inavunja sheria. tuache ubishoo wakuona kuwa kuna kazi ambazo hazikustahili wakati huna kazi ya kufanya.

Kuwa mbunifu, lakini pia tumia kipaji chako kujipatia kipato. usijilinganishe maisha yako na yawatu wengine, usiangalie watu waliofanikiwa bali angalia watu walio chini yako. mshukuru Mungu kwa uhai na uzima ulio nao. Fanya kazi kwa bidii ukimtanguliza Mungu utafanikiwa tu.