PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Monday, September 30, 2013

MAJI: TIBA KUBWA KULIKO ZOTE.:

Tuangalie ni kwa kiasi gani maji ni tiba kubwa kuliko zote mwilini. Mwili wa binadamu unategemea maji kwa kiasi kikubwa na unapokosa au kupungikiwa, hutoa ishara zake ambazo wengi wetu hatuzijui. Ishara hizo zinapopuuzwa huzaa matatizo mengine ya kiafya.

Kwa uchache, binadamu anatakiwa kunywa maji yasiyopungua glasi nane kila siku. Kiwango hicho kitaongezeka iwapo mtu ana uzito mkubwa na shughuli zake nyingi zinatumia maji mengi mwilini. Hivyo kiasi hicho cha glasi nane ni kiwango cha chini kabisa anachotakiwa kunywa mtu hata kama hana kazi yoyote.

Ifuatayo ni orodha ya magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa kunywa maji. Vile vile utajua baadhi ya dalili na madhara yanayojitokeza mwili unapoendelea kukosa maji:

1: Maji hutibu kiungulia (heart burn)
Kiungulia ni dalili kwamba mwili una upungufu mkubwa wa maji. Mara nyingi watu wanaposumbuliwa na kiungulia hudhani tumbo limejaa gesi hivyo kukimbilia kumeza vidonge ili kutuliza maumivu, lakini tatizo la upungufu wa maji huendelea kuwepo.

Bila kujua kuwa kiungulia kinatokana na kutokunywa maji, mtu huyo huendelea kumeza vidonge. Matokeo yake hali ya upungufu wa maji inapoendelea kwa muda mrefu, husababisha madhara mengine kama kuvimba tumbo, henia, vidonda vya tumbo na hatimaye kupatwa na saratani ya tumbo, maini na mapafu.

2: Maji hutibu baridi yabisi (Arthritis)
Maumivu ya kwenye mauingio ya mwili (baridi yabisi), hasa magoti, ni dalili nyingine ya upungufu wa maji katika sehemu hizo. Ni ugonjwa unaoweza kumpata mtu mzima na mtoto. Umezaji wa vidonge vya kupunguza maumivu hakuondoi tatizo, bali hufanya hali kuwa mbaya. Kunywa maji mengi na chumvi kidogo kunaweza kuliondoa tatizo kabisa.

3: Maji huzuia na kutibu maumivu ya mgongo
Maumivu ya kiuno na uti wa mgongo nayo ni dalili ya upungufu wa maji katika sehemu hizo, hasa katika maungio ambayo yanabeba uzito wa mwili. Maumivu ya aina hii hutibiwa kwa kuongeza kiwango cha kunywa maji na siyo madawa.

Mtu akiendelea kunywa dawa za kupunguza maumivu bila kuongeza kiwango cha maji mwilini, madhara yake huwa makubwa. Viungo huendelea kuathirika na hatimaye kudhurika kabisa na hivyo kumsababishia mtu ulemavu au upasuaji ambao humuachia maumivu siku zote yatakayomfanya kuwa mtumwa wa dawa.

4: Maji hutibu maumivu ya moyo (Angina)
Maumivu ya moyo nayo huwa ni dalili ya upungufu wa maji katika njia ya moyo na mapafu. Hali hiyo inapotokea, inatakiwa kutibiwa kwa kunywa maji mengi kila siku na siyo kukimbila kunywa dawa za kutuliza maumivu (pain killers).

No comments:

Post a Comment