PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Wednesday, June 26, 2013

Ujio wa Obama wasogeza ufunguzi wa sabasaba






Dar es Salaam. Ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya 37 ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (TanTrade), umesogezwa mbele kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Jackline Maleko, alisema maonyesho hayo yalitakiwa kufunguliwa Julai Mosi mwaka huu, lakini yamesogezwa mbele kupisha ujio wa Rais Obama na ule mkutano wa marais wa nchi wanachama wa Smart Patrnership.

Maleko alisema kutokana na hali hiyo, maonyesho hayo hayatafunguliwa siku hiyo, hadi wageni hao watakapoondoka nchini.

Alisema huenda yakafunguliwa kuanzia Julai 4 au 5, kulingana na ratiba itakayotolewa na Serikali.

“Ilikuwa tuzindue rasmi Julai Mosi, lakini tumebadilisha kutokana na ugeni wa viongozi hao, jambo ambalo mpaka sasa Serikali haijatoa taarifa rasmi ya tarehe maalumu ya ufunguzi huo,” alisema Maleko.

Maleko alisema kulingana na ratiba iliyopo, maonyesho hayo yatafunguliwa kama kawaida Juni 28, mwaka huu hadi Julai 8, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ndani na nje ya nchi.

Alisema kutokana na hali hiyo, wafanyabiashara wa ndani wanaweza kujenga mtandao wa biashara na wenzao wa nje, hiyo itawasaidia kupata masoko na kuongeza uzoefu.

Maleko alisema maonyesho ya mwaka huu, kutakuwa na bidhaa maalumu za ndani zitakazoonyeshwa kwa siku tofauti; asali, korosho na sanaa ya uchongaji.

Alisema lengo ni kutangaza soko la uzalishaji bidhaa hizo, jambo ambalo linaweza kuongeza masoko na kukuza mitaji kwa wazalishaji.

Pia, katika siku hizo, kutakuwa na siku maalumu ya kutangaza nembo ya Tanzania (Tanzania Brand) ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa sababu ndiyo muasisi wa siku nembo hiyo.Alisema tiketi za kuingilia kwenye maonyesho hayo zitaanza kuuzwa Juni 26.






No comments:

Post a Comment