PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

PATA POWER BANK ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KWA BEI NAFUU ZAIDI

Tuesday, June 25, 2013

Gharama za simu kupanda Julai


GHARAZA za huduma za simu kwa mtumiaji zinatarajiwa kuongezeka kuanzia Julai mosi mwaka huu.
Ongezeko hilo limetokana na serikali kuongeza kodi katika huduma za simu za mkononi.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania (MOAT) imesema pendekezo la serikali kutoza kodi kwa asilimia 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi haliwezi kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.
Kwa mujibu wa MOAT, awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwamba ongezeko la kufikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.
“Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha huduma za mawasiliano kuwa ni huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na kampuni za mawasiliano ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia,” inaeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Kampuni za Simu za Mkononi za Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel.
Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti katika Bara la Afrika, ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40.
MOAT ilisema mawasiliano ya simu si anasa, bali ni huduma muhimu katika Tanzania ya leo, sasa inakuwaje kuwatoza kodi mara kwa mara watu hao hao ambao wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao?

No comments:

Post a Comment